KOTEI ABATIZWA JINA LA MAGUFULI, AUNGANA NA STARS KESHO, AWAOMBA RADHI JUUKO NA OKWI
Kiungo matata Mghana anayekipiga katika klabu ya Simba, James Kotei, ameamua kuungana na watanzania kuishabikia timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kuelekea mechi ya kesho dhidi ya Uganda.
Mbali na kuwasapoti Stars, Kotei amewaomba radhi wachezaji wenzake Juuko Murushid na Emmanuel Okwi ambao wanaichezea Uganda.
Stars itashuka dimbani kesho kucheza mchezo wa kufuzu kuelekea AFCON na The Cranes majira ya saa 1:00 za usiku.
0 COMMENTS:
Post a Comment