March 23, 2019

MCHAMBUZI wa michezo bongo, aliyejipatia umaarufu kutokana na uchambuzi wake wa hisabati pamoja na kanuni kali ambazo zinawavutia waskilizaji na watazamaji, Mwalimu Kashasha amesema mashabiki wa Tanzania wasahau kuhusu kupata mteremko wa ujirani kwa mchezo wa kesho dhidi ya Uganda.

Kashasha amesema linapokuja suala la mechi za Taifa hakuna ambaye anakuwa na cha msalia mtume kwa mwenzio kutokana na thamani ya jezi ya timu ya Taifa.

"Ni ngumu kuamini kwamba wachezaji wa Uganda watatubeba licha ya kutokuwa na cha kupoteza, hivyo rai yangu kwa wachezaji wa timu ya Taifa kupambana mpaka tone la mwisho kupata matokeo, ugumu upo ila kuna mwangaza kwa timu kupaa matokeo.

"Hamasa ambayo imejitokeza kwa sasa naona kuna nguvu kubwa sana ya mashabiki ambao watajitokeza Uwanja wa Taifa hali hiyo itaongeza moto kwa wachezaji kucheza kwa kujituma kutafuta matokeo, ila wanapaswa waingie uwanjani wakiamini watashinda na sio ule ushindi wa kubebwa huo hautakuwepo kabisa," amesema Kashasha.

Stars inahitaji ushindi mbele ya Uganda ambayo kwenye mechi zote walizocheza hawajapoteza hata moja zaidi ya kutoka sare na Stars mchezo wa kwanza, tayari wameshafuzu kwenye kundi L kushiriki Afcon nchini Misri.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic