OKWI NA NYONI WAKICHAFUA VIBAYA BOCCO VETERANI LEO
Wachezaji wawili wa klabu ya Simba, mshambuliaji Emmanuel Okwi na beki Erasto Nyoni, leo wamefanya mazoezi ya pamoja katika viwanja vya Boko Veteran kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa klabu bingwa Afrika dhidi ya AS Vita Club ya DR Congo.
Okwi aliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Lipuli FC ya Iringa na alikosa mchezo dhidi ya JS Saoura Ugenini huku Erasto Nyoni aliumia kwenye michuano ya Mapinduzi Cup na kukosa mechi nne za Caf Champions League hatua ya makundi.
Wawili hao wanapewa nafasi kubwa ya kucheza dhidi ya AS Vita kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika Jumamosi ya wiki hii.
Kwa mujibu wa Daktari Mkuu wa Simba, Yassin Gembe, ameeleza maendeleo yao yanaenda vizuri na jukumu linabaki kwa Mwalimu kama anaweza akawapanga kwenye mechi hiyo.
Kama daktari amethibitisha , kocha hana uamuzi mwingine zaidi ya kuwapanga . Nyoni acheze beki ya kushoto ambapo shabalala na kwasi wapumue kidogo watacheza viporo vya ligi asiwe badala ya juuko
ReplyDeleteNyoni kucheza beki 3,bongela idea, hakika vita anakaa
ReplyDelete