March 13, 2019


KOCHA wa Lipuli, Seleman Matola amesema amejipanga kutibua mipango ya Yanga  kwa kuwa anawatambua vizuri wapinzani wake.

Yanga itashuka Uwajani Jumamosi huku wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza wa ligi waliocheza Uwanja wa Taifa kwa kupigwa bao 1-0.

Akizungumza na Saleh Jembe, Matola amesema amepata mbinu za kuimaliza Yanga kwenye mchezo wao utakaochezwa Uwanja wa Samora.

"Tupo imara na tuna nguvu ya kusonga mbele baada ya kupata ushindi mbele ya Mbao kinachofuata kwa sasa  ni kubeba pointi zetu kwa Yanga.

"Kila kitu kinawezekana na nimeawambia wachezaji namna bora ya kufanya kuibuka kidedea kwenye mchezo wetu tutakaokuwa nyumbani," amesema Matola.

2 COMMENTS:

  1. Duu na hii taarifa ya Lini mkuu

    ReplyDelete
  2. Mkiamini hivyo inawezekana pia ila sisi Wana Yanga zetu dakika 90, porojo hatuhitaji kabisaaaaaaa... Tumewachia wazee wa hamsa hamsa na nyie wafuasi wao

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic