March 15, 2019


MSHINDI wa milioni 123 za Perfect 12 ya M-Bet, Willy Wadson ametamba kwamba anaingia leo uwanjani kuitazama timu yake Simba kwa kulipa kiingilio maalum cha laki.

Willy amekuwa mshindi wa tatu wa Perfect 12 ya M-Bet baada ya kubashiri kwa usahihi timu 12 katika mkeka wake. 
Washindi wengine waliowahi kushinda Perfect 12 ni Frank Kayombo na Simoni Muray.

Mshindi huyo amejishindia kiasi cha milioni 123,614,160 kutoka Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya M-Bet.

Akizungumza na waandishi wa habari, Willy amesema atatumia kiasi cha fedha zake kwa ajili ya kwenda uwanjani kuitazama Simba leo Jumamosi wakati ikipambana na AS Vita katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar pamoja na kuboresha biashara yake.

"Kabla ya kushinda hii Perfect 12 nilikuwa ninataka kuja Dar kwa ajili ya kuitazama Simba ikicheza na Vita.

"Kwangu binafsi nimefurahi sana kuwa mshindi wa Perfect 12 ya M-Bet, nimekuwa nikicheza huu sasa mwaka wa tatu na kila siku natumia kiasi cha elfu 5000 ama zaidi.
Nimeshahinda huko nyuma lakini siyo kiasi kikubwa kama hiki.

"Mimi ni mkulima pia nafanya kazi ya kubadilisha fedha, hizi fedha nilizoshinda nitazitumia kwa ajili ya kuboresha biashara zangu na pia nitaangalia uwezekano wa kuwahamishia watoto wangu katika shule za kimataifa.

"Niwaambie Watanzania kwamba hizi fedha za ushindi kutoka M-Bet ni za kweli na ukishinda unapewa chako, hakuna suala la upendeleo hata kidogo," amesema Willy shabiki wa Simba na Manchester United.

Meneja Masoko wa M-Bet, Allen Mushi yeye amekazia kwa kusema: "Sisi M-Bet tukianza kuzimwanga tunazimwaga kweli huyu ni mshinidi wa tatu  sasa wa Perfect 12 zaidi ya milioni 500 zimetoka, kwetu dau linaongezeka kila siku pale inapotokea hatujampata mshindi.

"M-Bet ni walipaji kodi wazuri na katika kila mshindi anayepatikana basi hapo tunalipa kodi, kwa huyu Willy kuna kodi ya milioni 24 ambayo serikali inapata hivyo yeye atabakiwa na kiasi cha milioni 98," amesema Allen.

1 COMMENTS:

  1. M bet mnazingua nilipatia mechi 10 cha kushangaza mkanipa bonu tshs 1,850 hyo ni bonus kweli?nine bet kwa 1000/jackpot

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic