March 16, 2019


Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amekemea tukio la AS Vita kumpiga Mwandishi wa Habari kutoka gazeti la Championi, Ibrahim Mussa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara ameandika haya yafuatayo.

Hiki kitendo wa watu wa Vita kumpiga huyu kijana anayeonekana Mwandishi wa Habari siyo cha kiungwana na kinapaswa kilaaniwe!

Kwanini hawa watu wamepaniki kiwango hiki?

Sawa, nawasihi Wanasimba msirudishie ugomvi ili wasipate sababu ya kulalamika.

Twendeni tukamalizane nao kwenye Uwanja pale Taifa usiku wa leo.

Hawa ni jirani zetu ila washapagawa na wanajua hawatoki leo, tukutane kwa Mzee Mkapa 

Dor or Die

Na Haji S Manara

13 COMMENTS:

  1. Mbona wewe mwandishi ni kanjanja kiasi hicho?kwanini hukukemea kitendo cha mashabiki wa simba kulishambulia basi la AS VITA jana pale uwanja wa Taifa?Uandishi wa kijinga huu hautakufikisha mbali wewe na manara wote mazumbukuku na mtaona jinsi

    ReplyDelete
    Replies
    1. ACHA UFALA WEWE KWANI WEWE NI MCONGO?MBONA KISWAHILI CHAKO KIMENYOOKA KAMA CHURA KABISA

      Delete
  2. Basi gani lilishambuliwa?
    Wacha uzushi. Basi walilopaswa kutumia ni på Simba lakini walilikataa nä kikosi Coaster. Lile la Simba walikuwepo watu 6 tu ndani.Hakuna basi lililoshambuliwa wacha uzushi. Tunajua wazi ukuwadi unawasumbua. Badilisheni uraia muwe wakongo kwani husda na chuki zumewafanya vipofu.

    ReplyDelete
  3. Kiherehere chake alifata nn? Acha wamdunde tu.

    ReplyDelete
  4. Kiherehere chake alifata nn? Acha wamdunde tu.

    ReplyDelete
  5. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  6. Hivi uzalendo umepoteza tafsiri yake? Kwani Zana,Juuko, Wawa, Kotei, Kagere, Okwi na Chama ni raia wa Tanzania?
    Acheni hizoo, nyie pambaneni na hali yenu kama mnashinda shindeni kwa uwezo na yakiwakuta jueni kabisa yenu hayoo.
    Mwaka jana mwezi kama huu, wakati Yanga wanajiandaa kucheza na USM Algeirs, Haji aliwahi sema bora kushangilia jiwe kuliko Yanga; alibadilisha uraia?
    Kaka kila mchuma janga hula na wa kwao... lenu hilooo.
    Sema sana leo kwa sababu kesho utakuwa kimyaaa

    ReplyDelete
  7. Jackson umeshikwa kiuno huko Iringa bado mnahangaika na Simba.Simba kwa sasa sio level yenu.Mmeshangilia timu 4 za nje na wote walipewa kichapo huyu wa tano Leo zamu yake kuchapwa .
    Rudi hapa baada ya mechi udhihirishe ukuwadi wako.

    ReplyDelete
  8. Acheni kuingia na matokeo mfukoni, yasipoonekana mtang'oa miundombinu.....jueni Vita nao wamekuja na malengo ya kushinda. Niwasihi muwe mashabiki mnaojua possibilities 3 za matoke uwanjani...........win.....droo.....loose

    ReplyDelete
  9. Jackson rudini hapa mkazie mlichoandika.
    This is SIMBA. Tukiahidi tunatimiza. Sisi sio kama nyinyi walugaluga wakufungwa nyumbani.

    ReplyDelete
  10. Bwana Kaka kushinda mmeshinda lakini sisi hatuwezi kuwapongeza wala kufurahia, hilo ni la kwenu kuleni na wa kwenu!
    Hatutaki mtuombe ushirika kwa mgongo wa uzalendo, hilo halipo.
    Nyinyi kwa miaka minne mfululizo mmezishangilia timu ngapi za kigeni; mlikosa aibu hadi mkaishangilia timu ya Commoro? Ushirika haupo na msiutegemee.
    Nikukumbushe tu moja ya nukuu za Manara aliyoitoa mwaka jana "kun fay khoun"...kwamba kila mtenda hutendwa. Namalizia kwa shairi la Shabaan Robert "usifurahi mwanzoni"

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic