March 7, 2019



KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa kikosi cha Simba kina mtambo mkubwa wa wachezaji ambao wakitumika kwenye nafasi zao wataibeba kimataifa itakapocheza na JS Saoura ya Algeria.

Simba wametia timu Algeria wanatarajia kumenyana na JS Saoura kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa ikiwa ni hatua ya Makundi Jumamosi ya wiki hii Machi 9, 2019.

Zahera amesema kuwa kuna wachezaji ambao ni moto wa kuotea mbali ndani ya Simba wanakibeba kikosi hicho kutokana na uhalisia wao wa kupindua matokeo na kucheza kwa juhudi Uwanjani.

"Huyu Chama, (Claytous), Bocco (John), Kagere (Meddie) ni mfano wa wachezaji wenye nguvu na akili Uwanjani hawa wana uwezo wa kubadili matokeo na kuisaidia Simba kupata matokeo kimataifa, nafasi yao kutinga robo fainali kwa sasa ipo mikononi mwao.

"Ubora wa mchezaji upo kuanzia namna anavyotumia akili na nguvu kutafuta mpira hasa muda akiwa nao mguuni ama amepoteza, hiki ndicho wanacho wachezaji wa Simba na wakitumia zaidi akili watatimiza jukumu la kuipeleka timu hatua ya robo fainali, " amesema Zahera.

Simba wapo kundi D kwenye hatua ya makundi wakiwa nafasi ya pili baada ya kujikusanyia pointi sita ambapo kinara wao ni Al Ahly akiwa na point saba, mpinzani wa Simba JS Saoura nafasi ya tatu ana pointi tano wa nne ni AS Vita ana pointi nne. 

2 COMMENTS:

  1. Sikubaliani kabisa na maono ya zahera , anamuna Bocco kwa pasi yake kwa Kagere na kuifunga yanga kuwa ndiyo bora . Niambie katika kikosi cha wachezaji 20 walioenda Algeria ukianzia na Aishi Manula (Tanzania one), Wawa (Sultani) , Mkude Simba ,Zana wa kupanda na kushuka na wengineo hata wanaoanzia benchi akina Niyonzima nani mbovu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic