KIUNGO Myumbulifu wa t
imu ya Simba, Haruna Niyonzima amesema kuwa kazi kubwa iliyopo kwa sasa kwa timu ni kuona namna gani itapata matokeo kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa hatua ya robo fainali ili kutimga hatua ya nusu fainali.
Niyonzima amesema kuwa wachezaji wa Simba wanatambua ugumu wa hatua inayofuata na kila mmoja akili zake ni kuona namna gani atapata matokeo hivyo ni wakati wao sasa kupeperusha bendera ya Simba kuelekea kwenye mafanikio.
"Tumepenya hatua ya robo fainali kutokana na morali ambayo tulikuwa nayo wachezaji, kushirikiana na kukubali kwamba tunaweza kufanya kitu kikubwa kwa ajili ya Simba na hatimaye tumepata matokeo.
"Kwa sasa hakuna kingine tunachokifikiria zaidi ya kuona timu inapata matokeo kwenye hatua ya robo fainali ambayo tumepambana kuifikia na tumefanikiwa, mashabiki waendelee kutupa sapoti kwani uwepo wao umetusaidia kwa kiasi kikubwa," amesema Niyonzima.
Simba watamenyana na TP Mazembe kwenye mchezo wao utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Aprili 5 mwaka huu na watarudiana na Mazembe Congo baada ya siku sita.
Kumbuka kuna pingamizi CAF toka VITA na uchunguzi umeanza. VITA wanataka wapewe nafasi ya Simba. Soma kick off website na Ghana soccer net
ReplyDeleteChura husda zitawaua. Kila siku mpo na mambo ya Simba. Ya kwenu yamewashinda. Kutaka apewe nafasi sio siti za basi hizo. Wanaoshinda ndio wanaocheza hatua inayofuata.Yanga wasaidieni kukataa rufaa.
ReplyDeleteHakuna kitu km hicho
ReplyDelete