March 17, 2019


MASHABIKI wa Yanga wanamtamani, straika wa AS Vita, Jean Makusu lakini Kocha Mwinyi Zahera amewaambia hata wasihangaike kwa vile ni kazi bure. Zahera amekwenda mbali zaidi kwa kusema kwamba hata hao Simba wanaomnyemelea hawawezi kumpata kwavile hawezi kuja Tanzania kwa namna yoyote ile.

Kocha huyo akizungumza kwenye ofisi za Spoti Xtra zilizopo Sinza Mori, Jijini Dar es Salaam hivi karibuni, alisema kwamba atakuwa muongo kama akiwapa matumaini mashabiki ya kumpata mchezaji huyo ghali.

Zahera anamnoa mchezaji huyo kwenye timu ya Taifa ya DR Congo na Spoti Xtra linajua ni miongoni mwa
marafiki zake wakubwa. Kocha huyo alisema kwamba hata akilipwa Dola 30,000(Sh.70 Milioni) hawezi kuja Tanzania kwa vile miundombinu na vitu vingi ni vya hovyo.

“Leo hii nikisema namuhitaji Makusu katika kikosi changu nitakuwa muongo hata kama ni mwakani haitawezekana sababu hatuna fedha za kusajili na aweze kuja hapa Tanzania hata Simba na wakimtaka hawezi kuja.

“Halafu mimi ninamfahamu vizuri Makusu hawezi kukubali kuja kucheza huku Tanzania kwenye viwanja hivi vibovu eti akacheze huku sijui Singida mnaweza kumpa hata dola 30,000 akachukua na asije.

“Hatakuwa tayari kuona anaumia au anasafiri kwa masaa mengi na basi kwenda kucheza huku mikoani sidhani kama anaweza kuja,”alisema Zahera ambaye mashabiki wa Simba wanamlaani kwa madai kwamba amewasaidia AS Vita kwenye mechi ya jana usiku.

Makusu ni miongoni mwa wachezaji nyota wanaocheza ligi ya ndani ya Congo maarufu kama Linafoot na habari za ndani zinadai kwamba tayari ameshaingia makubaliano na klabu moja ya Morocco na huenda akajiunga nayo baadae mwaka huu.

Habari zinasema kwamba AS Vita wameshamalizana na klabu hiyo lakini bado hawajaweka mambo hadharani ila Zahera ameshaambiwa ukweli na Kocha wa Vita, Florent Ibenge ambaye wanaishi nae mtaa mmoja Ufaransa na ni bosi wake timu ya Taifa.

Ibenge amewaambia Simba kwamba kama wakimsajili Makusu yeye atamchukua Meddie Kagere kwa dau lolote lile. Zahera tangu atue Yanga alimsajili kipa Klaus Kindoki na straika Heritier Makambo na wote kutoka DR Congo.

Kwa mujibu wa mtandao unaohusika na ishu za usajili duniani wa Transfer Markt wa Ujerumani, thamani ya Makusu ni zaidi ya Sh.357milioni. Thamani hiyo inatokana na umri mdogo wa mchezaji huyo ambao ni 26 pamoja na ufanisi wake.

4 COMMENTS:

  1. Kauli ya Zahera kwamba Makusu awezi kuja kucheza timu yoyote Tanzania eti kwa sababu miundo mbinu ya viwanja na barabara huku TZ ni mibovu ni UONGO ULIOPITILIZA. Ebu tu angalia uwanja mkuu wa DRC kisha ulinganishe na kwa mkapa utaona kuwa wa kwetu ni mzuri zaidi na wa kisasa sana. Achilia mbali uwanja mpya wa Taifa utakaoanza kujengwa Dodoma wa kiwango ambach DRC haitoweza kuwa nao kwa miaka zaidi ya 30 ijayo sbb uchumi na maisha ya DRC yako chini sana kwa sbb ya vita, rushwa zilizokithiri na uongozi mbovu. Hakuna miundo mbinu mizuri ya barabara, hakuna hospital hakuna amani. Hakuna benki, hakuna hata chakuka cha kutosha. Hakuna kila kitu ndio maana wacongo wengi akiwemo yeye Zahera wanakimbia nchi yao na kuishi ugenini anakodai eti hakufai. Tanzania ingekuwa mbaya usingemuona Zahera hapa wala Kindoki wala wale wakongo waliokuja kuomba kazi Simba mwaka juzi na kushindwa kufuzu majaribio na kushindwa. Kuna wacongo wengi wanakimbia DRC sbb ni kubaya. Uwezi kuona watz wanakimbia tz kwenda kutafuta maisha DRC.
    Kwanza huyo mvhezaji mwenyewe hana kiwango cha kuchezea Simba ndio maana ameshindwa kuthibitisha ubora wake dhidi ya simba ktk siku na kipindi muhimu zaidi kwa timu yake. Sio mchezaji wa kutehemewa timu ya taifa ya DRC ambayo.ilipigwa goli 2 na Taifa Stars na timu yao ya vijana nayo.pia ililigwa na timu ywt ya vijana na kutolewa kwemye mashidano. Ubora wa Makusu uko wapi? Kagere ana goli nyingi CAF kuliko Makusu

    ReplyDelete
  2. Hatoweza kutuwa Yanga kwakutegemea bakuli lakini atatuwa kulikonona bwanazzzmoo

    ReplyDelete
  3. Huyo Zahera hana lolote, nchi zetu hizi za ukaenda huu viwanja vyetu havitofautiani sana sasa anaposema viwanja vibovu na Usafiri wa muda mrefu anabwabwaja tu na yote ni Wivu kwa kutaisha watu tamaa, pia nimekuona ni Mtu anayetutangaza vibaya Tanzania lakini bado anaweka mashavu yake nchini, ligi mbovu ondoka katafute ligi nzuri na yenye viwanja vizuri sio kubwabwaja tu ...

    ReplyDelete
  4. Zahera atambue kwamba mo amewekeza simba kwa hisa ya 49% (20 bil) , tukimhitaji hata mesi atatua msimbazi , ndiyo tushindwe kwa huyo makusu wake wa dola 30,000 (mil 70)

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic