April 28, 2019


Haruna Niyonzima kiungo wa Simba amewaomba radhi mashabiki wa Simba pamoja na uongozi baada ya jana kuonyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi.

Jana wakati Simba inabeba pointi tatu uwanja wa Karume mbele ya Biashara United alitolewa kwa kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya kuwa na kadi mbili za njano kwenye mchezo huo uliokuwa na mikikimikiki.

"Ulikuwa ni mchezo wenye presha kubwa na nguvu nyingi, tulihitaji matokeo kwa namna yoyote, iliniumiza sana kuona timu yangu inamaliza tukiwa pungufu, niombea radhi kwa klabu yangu, mashabiki walioongozana na timu pamoja na wale waliotazama mchezo kupitia luninga zao.

"Nilichokifanya hakikuwa bora kwa ustawi wa mpira ila tutapambana mpaka mwisho kufikia malengo yetu ya kutetea ubingwa," amesema Niyonzima.



2 COMMENTS:

  1. Ukomavu mkubwa wa kukubali kosa.Ni matarajio ya wanasimba kwamba umejifunza. Kila la kheri Fundi.

    ReplyDelete
  2. ujinga wakati nahodha wako anakuzuia wewe bado ulikuwa mbishi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic