May 20, 2019


UONGOZI wa Singida United umesema kuwa kiungo wao Keny Ally kwa sasa yupo huru kuzungumza na timu yoyote hivyo kama Yanga wanahitaji huduma yake milango ipo wazi.

Ally alikuwa kwenye hesabu za kocha Mwinyi Zahera wakati wa dirisha dogo dili hilo liliyeyuka kutokana na viongozi ambao aliwapa kazi ya kumsajili kushindwa kutimiza masharti yake.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema kuwa wanaskia kwamba Yanga wanahitaji saini ya mchezaji wake ila kwa sasa hakuna ambaye amewafuata.

"Unajua kwa sasa Ally mkataba wake unakamilika msimu unapoisha, utaratibu unamruhusu kuzungumza na timu ambayo inahitaji saini yake, sasa kama Yanga wanahitaji saini yake nafasi ipo wazi," amesema Katemana.

Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kwamba anatambua mashabiki wa Yanga wanapenda kuona timu inakuwa bora ila kwa mpango wake ulivyo wenyewe watafurahi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic