May 2, 2019

UONGOZI wa Azam FC, umesema kuwa kesho watalipa kisasi chao cha kupoteza mbele ya Yanga mchezo wa Ligi Kuu Bara kwa kuibuka na ushindi mbele ya kikosi cha KMC.

Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga, amesema kuwa wanaitambua KMC ila kesho watawasamehe bure kwa kuwa wamejipanga kushinda ili kutinga hatua ya fainali ya kombe la Shirikisho.

"Ni mchezo mgumu wa hatua ya mtoano, tunatambua kwamba ni lazima mshindi apatikane kwa kuwa ni nusu fainali, sasa kama tutakwa nyumbani na tumejipanga basi tunahitaji ushindi hakuna kitu kingine.

"Malengo yetu ni kuona tunaibuka wababe na kutinga hatua ya fainali hakuna jambo lingine zaidi, hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kuona namna mchezo utakavyokuwa," amesema Maganga.

Timu zote mbili zimetinga hatua ya nusu fainali kombe la FA kwa mara ya kwanza uwanja wa Chamazi majira ya saa 1:00 usiku na mshindi atakutana fainali na Yanga ama Lipuli.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic