May 2, 2019

USHINDI walioupata leo Yanga wa mabao 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons uwanja wa Uhuru wamedhihirisha kwamba kwa sasa ni lazima kila mmoja ashinde mechi zake huku ngoma ikiwa bado mbinchi.

Heritier Makambo dakika ya 66 alifunga bao ambalo limeipa pointi tatu Yanga baada ya lile la kwanza kufungwa na Pappy Tshishimbi dakika ya 23 kusawazishwa na Ismail Kada wa Prisons dakika ya 33.

Makambo anaongeza moto wa vita ya Ufungaji bora bara baada ya kuwafikia, Meddie Kagere wa Simba na Salum Aiyee wa Mwadui FC ambao wote kwa sasa wana mabao 16.

Yanga wanajikita kileleni wakiwa na pointi 80 huku Tanzania Prisons wakibaki na pointi zao 42 wakiwa nafasi yao ya nane baada ya kucheza michezo 33.

Huu ni ushindi wao wa pili uwanja wa Uhuru, walianza kushinda mbele ya Azam FC kabla ya leo kuibuka kidedea dhidi ya Prisons.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic