UONGOZI wa Ruvu Shooting umesema kuwa kesho unazindua rasmi mtindo wao wa 'MpapasoSquare' kwa kuwapapasa wanajeshi wa JKT Tanzania ikiwa ni dabi ya wanajeshi.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema wamekuwa wakipata taabu sana kupata matokeo msimu huu kutokana na ushindani uliopo kwa sasa ndani ya TPL.
"Ligi kuu kwa sasa ni moto ila kesho ni lazima tuzindue mpango wetu na sera yetu ya 'Mpapaso Square' kwa JKT Tanzania kisha baada ya hapo tutajua ni namna gani tutafanya mechi zetu zinazofuata.
"Hawa ni wanajeshi wenzetu, JKT, sasa mbinu zetu zinafanana, tumejipanga kuwaonesha namna gani tupo imara na kamili gado kubaki kwenye ligi msimu ujao, mashabiki wajitokeze kwa wingi, uwanja wa Mabatini," amesema Bwire.
Ruvu Shooting wapo kwenye mstari mwekundu kwa sasa baada ya kucheza michezo 33 wapo nafasi ya 19 wakiwa wamejikusanyia pointi 36 kibindoni.

0 COMMENTS:
Post a Comment