May 18, 2019


LICHA ya Mtibwa Sugar kutofungwa na mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere, uongozi umesema kuwa Kagere sio mtu mzuri kwani aliisumbua safu yao ya ulinzi mwanzo mwisho.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa matokeo ya mabao 3-0 waliyoyapata uwanja wa Uhuru ni mabaya na yanasikitisha ila safu ya ushambuliaji wa Simba iliwapa taabu sana.

"Tumefungwa kwa sababu ya makosa yetu, Simba wametupotezea malengo yetu ya kutwaa pointi tatu, kiukweli safu yao ya ushambuliaji inayoongozwa na Kagere sio watu wazuri hivyo tunakwenda Morogoro tutapindua matokeo.

"Wameshinda mchezo wao wa kwanza msimu huu wakiwa nyumbani, wakija nyumbani lazima tulipe kisasi kwani kikosi chetu hakikucheza katika kiwango ambacho tumekizoea kwenye michezo yetu ya nyuma," amesema Kifaru.

Mtibwa Sugar itarudiana na Simba mchezo wa mwisho utakaochezwa uwanja wa Jamhuri Morogoro, Mei 28. Kagere kwenye mchezo wa juzi alitoa pasi ya bao lililofungwa na John Bocco.
Azam yaipa Simba ubingwa

1 COMMENTS:

  1. tunahitaji akina kidaru tobias waongee mpira sio kina zehra kila wanapo kosa matokeo wanaleta visingizio mara rifa mata tff mara watani wanabebwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic