KASHASHA: CHAMA HATADUMU SIMBA, ANACHEZA MPIRA WA MAJUKWAA – VIDEO
MCHAMBUZI wa masuala ya michezo, Alex Kashasha, ameichambua mechi ya Ligi Kuu kati ya Simba na Mtibwa Sugar iliyochezwa jana Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na kusema mchezaji Clatous Chama hawezi kudumu Simba kwa sababu anacheza mpira wa majukwaa wa kujionyesha kwa mashabiki, hivyo akikosolewa atachukia.
Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0, hivyo kuirejesha kileleni kwa kuishusha Yanga ambayo ilikuwa inaongoza baada ya kufikisha jumla ya pointi 83 huku Simba ikifikisha jumla ya pointi 85.
Simba wana pointi 84 na mabao 72, kinara wa mabao akiwa ni Meddie Kagere mwenye mabao 20.
Timu hiyo ya mtaa wa Msimbazi, Kariakoo, jijini Dar es Salaam ina michezo minne mkononi ili kukamilisha ligi ya msimu huu, ikitakiwa kuwa na pointi tano ili kutetea ubingwa wake.
Upo sahihi kabisa mwalimu Kashasha,na sio yeye tu hata Niyonzima ndo kabisaaa.Najua mashabiki wa Simba watachukia kuambiwa ukweli huu lakini ndo ukweli wenyewe
ReplyDeleteNI KWELI KABISA CHAMA AAMBIWE SISI HATUTAKI MPIRA WA SHHOO OOFFF TUTAMCHUKIA SASA HIVI. MTU ANAPIGA CHENGA MPAKA GOLINI HALAFU ANAGEUZ MIRA KURUDISHA NYUMA BADALA YA KUFUNGA. TUNATAKA MAGOLI HATA YAWE 10. ANAYEJUA KIINGEREZA AMWAMBIE CHAMA .... WE DONT WANT SHOW OFF GAME WITH LOT OF DRIBLING AND WASTAGE OF CLEAR CHANCES TO SCORE GOALS. WE RESPECT YOU MR. CHAMA, WE LOVE YOU BUT WHEN YOU PLAY SHOW OFF GAMES WE GET DISAPPOINTED. WE NEED GOALS NOT SHOW OFF GAMES.
ReplyDeleteKashasha abaki kuchambua mpira atuachie chama wetu wanaocheza na jukwaa ni Ajibu na Nyinzima
ReplyDelete