MSHAMBULIAJI wa kikosi cha Azam FC, Obrey Chirwa ameusubirisha mkataba wake wa kwenda Simba baada ya kuwaambia viongozi wa Azam FC kwamba atakaa mezani kuzungumza nao kama atabaki ama kuondoka baada ya msimu kuisha.
Chirwa amekuwa akihusishwa kujiunga na kikosi cha Simba tangu msimu uliopita ila aliwakimbia mabosi hao na kujiunga na timu ya Misri kabla ya kuibukia kwa matajiri wa Dar, Azam FC.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mratibu wa Azam FC, Philip Alando amesema kuwa uongozi ulizungumza na Chirwa juu ya kuongeza mkataba wake ila amewaambia wasubiri mpaka msimu uishe.
"Chirwa tulikuwa na mpango wa kumuongezea mkataba ila ametuambia kwamba tusubiri mpaka ligi iishe, nasi pia tunaheshimu mawazo yake ligi ikiisha tutazungumza naye tujue hatma yake.
"Kwa sasa bado hatujapata ofa inayomtaka yeye kuondoka hivyo kama ikitokea maamuzi ni yake maana mchezaji kazi yake ni mpira atakuwa huru kujiunga na timu ambayo ataichagua," amesema Alando.
0 COMMENTS:
Post a Comment