May 6, 2019


BEKI wa Simba, Zana Coulibaly raia wa Ivory Coast, jana alimwaga machozi wakati akitoka baada ya kufanyiwa mabadiliko dakika ya 90 na nafasi yake kuchukuliwa na Nicholas Gyan.

Ilikuwa ni katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara katika Uwanja wa Sokoine jijini hapa.

Coulibaly, hakutarajia kama atatolewa uwanjani, na alikuwa mzito kutoka alipopewa taarifa hizo.

Alipotoka, alikuwa akimwaga machozi na aligoma kumpa mkono kocha wake, Mbelgiji Patrick Aussems.

Alionekana kumkwepa lakini kocha huyo alimfuata, hata hivyo beki huyo aligoma kumpa mkono, na alipitiliza moja kwa moja hadi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.

1 COMMENTS:

  1. Si kweli acha kuandika uzushi Aussen alimpat kwenye bega.Hakuna mkono pale

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic