May 6, 2019


WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, ameweka wazi kwamba kabla ya kufanyika uchaguzi wa Klabu ya Yanga jana Jumapili, alishawahi kupigiwa simu na watu wengi ambao wengine walimpa lugha kali zisizoelezeka ikiwa ni baada ya viongozi waliokuwepo madarakani akiwemo mwenyekiti Yusuf Manji, kujizulu.

Mkuchika alikuwa mmoja wa wanachama wa Yanga ambao walijitokeza jana katika uchaguzi mkuu wa Yanga wa kuwachugua mwenyekiti, makamu mwenyekiti na wajumbe uliofanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay jijini Dar.

Yanga ilifanya uchaguzi wake ikiwa ni baada ya viongozi wa klabu hiyo wakiongozwa na Manji, makamu mwenyekiti, Clement Sanga na wajumbe wa kamati ya utendaji kujiuzulu nafasi zao.

Mkuchika amesema kwamba alikuwa anatolewa lugha hizo kali kupitia njia ya simu wakati ambao klabu hiyo haikuwa na viongozi na uchaguzi ulikuwa bado haujafanyika.

“Ninawaomba Wanayanga leo (jana) wasifanye makosa, wachague viongozi wazuri ambao watatuendeshea vizuri klabu kwa miaka minne ijayo.

“Nakumbuka kipindi cha mchakato wa uchaguzi huu ilifika wakati ninapigiwa simu na watu ambao walikuwa wanatoa lugha kali wakiwa wanaulizia juu ya uchaguzi huu, sasa hii ni nafasi kwenu, msifanye makosa,” alisema Mkuchika.

2 COMMENTS:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Uongozi mpya wa Yanga utathmini maendeleo na kwanini timu haijafanikiwa....ingawa ni kweli kuwa huyo kocha amewasaidia lakini lazima kuwepo na kubadilishwa na kuliimarisha benchi zima la ufundi...msiridhike kwakuwa mnaongoza ligi na mmefikia nusu fainali ya FA. Ukweli ni kwamba timu ina mapungufu mengi sana....caliber ya wachezaji wa Yanga wengine hawakufaa kuwemo kwenye hii timu wengi wao viwango ni vya chini mno, na umri umesogea mno. Pia mwalimu wa viungo, kocha wa makipa, madaktari, mameneja na wachua misuli....bado ni wa level ya chini hawana tofauti na wa timu za Ndanda, Alliance nk....usajili na viwango vya professional players ni duni....ndio unaweza ukadai kuwa tatizo ni pesa lakini hata hivyo baadhi yao hata scouting was very poor, na hawakuwa fiti, kuporomoka kwa uchezaji wao na umri umesogea mno, wachezaji wengi wazawa pia kuna kushuka kwa viwango kama ilivyo kwa wageni......timu kama Lipuli siyo ya kuitoa Yanga....yaliyopita si ndwele sasa nyinyi yeboyebo mugange yajayo....USAJILI WA KIWANGO CHA JUU NA KULIIMARISHA BENCHI LA UFUNDI....Challenge ni kushawishi wachezaji waliopo ambao wameibeba timu kubaki kikosini....kwa kusaini mikataba mipya!....Kuhusu Uwezo wa Mwalimu Noeli Mwandila....sidhani kama unaridhisha....kila ambapo Mwalimu Zahera akiondoka kwenda kwenye timu ya Taifa Kongo....akirudi viwango vya wachezaji vinakuwa chini mno....physical fitness is very low!...lazima ili liangaliwe....madaktari pia wachezaji walio majeruhi Yanga huchukua muda mrefu kupona....nadhani kuna haja ya kuipa uwezo na vifaa vya kisasa idara ya utabibu....yako madhaifu mengi mfano mengine kama kutokuwepo kwa ubora wa kambi na viwanja vya mazoezi, na kadhalika lakini haya ndio ya msingi....sasa mengine yalichangiwa na uongozi dhaifu na uchumi kudorora sasa hivi au msimu ujao hilo lisiwe tena kisingizio!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic