May 1, 2019


BAADA ya kampeni za Uchaguzi wa Yanga kuzinduliwa jana, mgombea wa nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji Yanga, Saady Khimji ameahidi kuboresha mfumo wa uendeshaji ndani ya Yanga endapo atapata nafasi hiyo.
Khimji amesema kuwa ana uzoefu mkubwa wa uongozi na anatambua uhitaji wa wanachama wa Yanga kutokana na kuwa karibu na chama hivyo anaamini akipata nafasi atatumia uzoefu wake kubadili mfumo.
"Nina uzoefu kwenye masuala ya uongozi pia ninaitambua vema Yanga hivyo wanachama wakinichagua hawatajutia nitafanya kwa vitendo na nitaongeza mshikamano ambao upo kwa sasa ndani ya Yanga hasa kwa kuwekeza.
"Unajua Yanga ni klabu kubwa na ina vyanzo vingi vya mapato kwa kushirikiana na wenzangu tutabuni miradi inayotelezeka itakayovutia wadhamini, pia kupitia mshikamano itasaidia kuendeleza rekodi ya kubeba makombe pamoja na kuwa na Yanga bora," amesema Khimji ambaye ni diwani wa Kata ya Ilala.

1 COMMENTS:

  1. Watu wa kuunga juhudi tusiwape nafasi, endelea na Siasa, WANASIASA ndio wametufikisha hapa,tusiwape nafasi kwenye Uongozi huu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic