May 1, 2019

KOCHA Mkuu wa timu ya Simba, Patrick Aussems amesema kuwa ilikuwa ngumu kwake kupata matokeo mbele ya JKT Tanzania jana kwani alikata tamaa kutokana na wapinzani wao kuwa makini muda wote.

Akizungumza na Saleh Jembe, Aussems alisema kuwa mpira ni mchezo wa makosa kama wapinzani hawatafanya makosa inakuwa ngumu kupata matokeo hali iliyomfanya adhani kwamba atavuna pointi moja.

"Unajua mpira ni mchezo wa makosa, nilikuwa naangalia namna wapinzani wetu walivyokuwa wakifanya kazi kubwa kusahihisha makosa yao nikajua tu hapa kazi ni ngumu, ila ajabu kosa moja limewagaharimu tumepata matokeo.

"Haikuwa rahisi na haikuwa ngumu ila yote ni matokeo, kwangu naona ni furaha pamoja na mashabiki kwa kuwa tumepata pointi tatu tutafanyia kazi makosa ambayo tumeyafanya," amesema Aussems.

Simba ilishinda bao la usiku dakika ya 90+6 kupitia kwa Hassan Dilunga akimalizia pasi ya Emmanuel Okwi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic