MENEJA wa Real Madrid, Zinadine Zidane ameshindwa kuwa na msimu mzuri baada ya kurejea kwenye klabu yake ya zamani ambayo aliiacha kwa mafanikio makubwa.
Zidane amejikusanyia jumla ya pointi 17 kwenye michezo yake 11 ya mwisho ya msimu, na mchezo wake wa mwisho alipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 mbele ya Real Betis.
Mchezo huu unawafanya Real Madrid kuanza kujipanga kwa ajili ya msimu ujao huku Gareth Bale akiwa kwenye shinikizo la kuachwa na uongozi kutokana na kushindwa kuonyesha uwezo mkubwa msimu huu.
Meneja huyo raia wa Ufaransa alikuwa anahitaji kutumia michezo yake ya mwisho 11 kwa ajili ya kujipanga msimu ujao baada ya kupokea kijiti kutoka kwa Santiago Solari, na amemaliza vibaya kuliko ilivyotarajiwa.
.
0 COMMENTS:
Post a Comment