May 19, 2019


VINCENT Kompany mchezaji wa Manchester City amesema atajiunga na klabu ya Anderlecht ambayo ilikuwa ni klabu yake zamani alipokuwa na miaka sita akiwa ni kocha mchezaji ikiwa ni kitu ambacho alikuwa anapenda zaidi kukifanya.
Kompany mwenye umri wa miaka 33 amesaini dili la miaka mitatu ndani ya klabu hiyo ya Belgian baada ya miaka 11 kuitumikia akiwa ndani ya uwanja wa Etihad na ametumia miaka nane kuongoza timu akiwa ni nahodha.
Mchezo wa jana dhidi ya Watford uwanja wa Wembley ulikuwa ni wa mwisho kwa nahodha huyo ambao walitwaa kombe kwa ushindi wa jumla ya mabao 6-0 baada ya kushinda kombe la Ligi Kuu England wakiwa na pointi 98.
"Idadi kubwa ya muda ambao nimetumika timu ya City nilikuwa naifikiria siku ya namna hii, baada ya yote sasa yanatimia.
"Man City wamenipa mimi kila kitu na nilijitahidi kwa kila namna kurejesha kwa uwezo wangu na kwa namna nilivyoweza, nahitaji kuwashirikisha wengine ujuzi wangu kwa manufaa ya kizazi kijacho" amesema Kompany.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic