May 19, 2019


KOCHA wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa timu ya Ndanda ni miongoni mwa timu ngumu kwenye Ligi Kuu Bara kutokana na mwenendo wake kwenye ligi hivyo anaingia uwanjani kwa tahadhari kubwa.

Leo Simba itawakaribisha Ndanda Uwanja wa Uhuru ambapo utakuwa ni mchezo wa pili wakiwa na kumbukumbu ya kugawana pointi moja mchezo wa kwanza Mtwara.

"Hapa leo nakutana na timu ngumu na bora kwani nimeifuatilia haipotezi michezo yake kiwepesi, safu yake ya ulinzi na aina ya wachezaji wake wapo vizuri, nawaheshimu ila tutacheza tukiwa ni timu kutafuta pointi tatu," amesema Aussems.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic