UONGOZI wa KMC umesema kuwa wapo tayari kwa mchezo wao wa hatua ya nusu fainali kombe la Shirikisho kesho dhidi ya Azam FC utakaochezwa majira ya saa 1:00 uwanja wa Chamazi.
Ofisa Habari wa Azam FC, Anwar Binde amesema kuwa hawana hofu na kikosi chao kutokana na maandalizi waliyoyafanya kuwakabili wapinzani wao.
"Tupo sawa na tayari tumeanza maandalizi ya kuchonga kabati kwa ajili ya kutwaa kombe la la FA, tumejipanga na tuna imani ya kupata matokeo.
"Morali ya wachezaji ni kubwa na kila mmoja yupo tayari kupata matokeo, hakuna namna yoyote ya kufanya zaidi ya kushinda, mashabiki wajitokeze kwa wingi," amesema Binde.
Msimu huu KMC wametinga hatua ya nusu fainali kwa mara ya kwanza kwenye kombe la FA kwani msimu uliopita waliishia hatua ya awali na walitolewa na Azam FC uwanja wa Chamazi.
0 COMMENTS:
Post a Comment