May 7, 2019


BADO gumzo kubwa kwenye ligi ni uwezo wa kiungo mshambuliaji wa timu ya Yanga, ambaye ni nahodha Ibrahimu Ajibu ambaye kwa sasa kasi yake ni ya ajabu akiwa uwanjani.

Amekuwa ni mchezaji anayehusishwa kurejea kwenye timu yake ya Zamani ya Simba ambapo amesema kuwa kwa timu itakayofuata utaratibu ataitumikia kwani kazi yake ni mpira.
Ajibu hapendi makuu kutokana na namna ambavyo anaishi na ndugu zake pamoja na familia kiujumla, mguu wake anaouamini ni wa kulia akiwa uwanjani na unafanya mambo mengi yaayowafanya wapinzani kulia.
Kwenye mabao 52 ambayo Yanga wamefunga amehusika katika jumla ya mabao 22 ambapo ametengeneza pasi za mwisho 17 na kufunga mabao 6, hali ambayo inadhihirisha kwamba ni injini ndani ya Yanga kwa namna anavyotimiza wajibu wake.
Ana mengi sana Ajibu anafuguka mipango yake kwa sasa pamoja na kilicho nyuma ya mafanikio yake,huyu hapa anafunguka:
"Kitu kikubwa ambacho kinanifanya niweze kuonekana bora ni muunganiko ndani ya kikosi chetu, kila mmoja anatimiza majukumu yake uwanjani hali inayofanya tupate matokeo.
"Hesabu kubwa ni kuweza kufanya kazi kwa uhakika na kufanikiwa kupata pointi tatu hicho ndio kipaumbele chetu kikubwa.
Ushindani wa ligi unauzungumziaje?
“Kila timu imejipanga kufanya vizuri nasi tumejipanga kufanya vizuri, nasi tunajua kazi yetu ni kutafuta matokeo uwanjani hakuna jambo lingine.
Huwa unafikiria nini ukiwa na mpira mguuni?
"Wenzangu ambao nipo nao pamoja na kuangalia mahali nilipo kama ni sahihi kuweza kufunga ama kuna mwenzangu ambaye anaweza kufunga.
Kwa nini huwa unakuwa hata kama mmeshinda?
"Lazami tuwekane sawa tukiwa uwanjani ili tusijisahau, mpira ni dakika 90 hivyo mpaka zikamilike hapo tunajua tumemaliza kazi ila kama bado tunaendelea hatupaswi kutulia.

Mafanikio yako je?
"Ushirikiano uliopo ndani ya timu, kila mmoja anafanya kazi yake kwa ufanisi, namshukuru Mungu pia kwa haya.
Mwalimu akiwa anakuchana kwamba hauna uwezo inakuaje kwako?
"Sina muda wa kufuatilia maneno ya mwalimu wangu kwa ubaya hasa kutokana na namna ambavyo ananisema, hayanipi wasiwasi wala kuongeza chuki bali yananipa hasira zaidi ya kupambana.

Kuondoka kwako Yanga je?
"Kwangu mimi ni sawa kwa kuwa mpira ni kazi yangu, timu ambayo inanifuatilia ikifuata utaratibu naitumikia sina tatizo lolote.
"Jambo jema hasa kwa kuwa natafuta mafanikio ndani ya mpira na nikipata timu nyingine nje ya nchi itakuwa ni fursa kwangu kuonyesha uwezo wangu na kufanya kazi zaidi ya hapa nilipo, ila kwa sasa bado nipo Yanga," anamaliza.
Meneja wa Ibrahimu Ajibu ambaye ni ndugu yake Athumani Ajibu amesema kuwa uwezo wa Ajibu ni mkubwa na anaamini mengi yanakuja kwake.
"Kuna timu nyingi ambazo zinamfuatilia Ajibu hasa kutokana na uwezo wake kuwa juu kwa sasa, bado ana    mkataba na Yanga ambao nao pia wana hitaji huduma yake baada ya mkataba wake kuisha hivyo ni jambo la kusubiri," alisema.

2 COMMENTS:

  1. Reality unajua. Sio mbaya ukosepa poa ukibaki poa ni namna tyu ya kusaka maisha

    ReplyDelete
  2. Umesaini simba tuu,mpaka unaitwa timu ya taifa hilo no la kujiuliza Sana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic