May 17, 2019


SIKU chache baada ya kufanikiwa kuvunja mkataba na Yanga, aliyekuwa kipa namba moja wa timu hiyo, Beno Kakolanya amewaomba radhi wapenzi na mashabiki wa timu hiyo.

Ikumbukwe kuwa Kakolanya alifi kia hatua hiyo ya kuomba aachwe na Yanga ili akatafute maisha sehemu nyingine baada ya kocha mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera kugoma kufanya kazi naye kwa madai ya kuwa na utovu wa nidhamu, hata hivyo inadaiwa kuwa yupo karibuni kusaini Simba.

Kakolanya amewataka wapenzi na mashabiki wa Yanga wamsamehe kwa yote yaliyotokea kwani hakuwa na njia nyingine ya kufanya ili kuhakikisha analinda kipaji chake.

“Ni kweli kabisa hivi sasa mimi ni mchezaji huru na sina tena mkataba na Yanga kwani tayari umeshavunjwa na nishapewa barua inayoonyesha kuwa mimi ni mchezaji huru sasa.

“Hata hivyo, nimekuwa nikipokea simu mbalimbali kutoka kwa mashabiki wa Yanga wakinilaumu kuwa kuondoka kwangu ndiyo kumesababisha timu iwe hapo ilipo, ila naomba wajue kuwa siyo mimi niliyetaka niondoke.

“Lakini niwaombe tu msamaha kwa yote yaliyotokea kwani haya ni maisha tu, kwa hiyo haitapendeza kama kutakuwa na hali ya chuki dhidi yangu kutokana na hiki kilichotokea nafi kiri muda mchache mtafahamu nakwenda wapi,” alisema Kakolanya ambaye awali alikuwa kipa namba moja wa timu hiyo.

1 COMMENTS:

  1. TUMEKUSAMEHE NENDA SALAMA KUSEMA KWELI HUWEZI KUTUMIKIA TIMU HUKU HULIPWI MISHAHARA MIEZI NA MIEZI UKIDAI KOCHA ANAKUJA JUU ETI MBONA WENGINE PIA WANADAI SASA KWANI MAHITAJI YA BINADAMU NI SAWA? MWINGINE ANAUGULIWA MWINGINE AMEFIWA MUHIMU ULIPWE HAKI ZAKO. ILA UKWELI YANGA CHINI YA ZAHERA HATUJAKUMISS SANA KWAKUWA TIMU ILIBALANSI IMEPAMBANA MPAKA TUKAONGOZA LIGI. WEWE NENDA TUU HATUNA TATIZO TUTACHUKUA NAFASI YA KWANZA AU YA PILI KWENYE LIGI.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic