May 17, 2019


BODI ya Ligi iliyo chini ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imetoa tahadhari kwa timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu Bara ikiwemo Simba na Yanga kuwa makini katika mechi za mwisho na kusema kuwa inatuma watu maalumu kufuatilia mechi hizo ili kuepuka upangwaji wa matokeo.

Ligi inafikia tamati Mei 28 ambapo Simba imebakiza michezo mitano huku timu nyingine zikiwa zimebakiza michezo mitatu kukamilisha mzunguko wa ligi wa msimu wa 2018/19 ambapo hadi sasa bingwa bado hajajulikana.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Steven Mguto amesema kuwa, wanawatuma watu maalumu kufuatilia kila michezo inayochezwa kuanzia sasa ili kila timu ipate matokeo kulingana na jinsi inavyocheza.

“Suala la timu kulalamika lipo wazi hivyo tunahitaji kuwatuma watu maalumu kuweza kufuatilia mechi zitakazochezwa kwa kuwaongezea wale waliokuwepo ili kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa nakuepuka upangwaji wa matokeo.

“Vile vile mechi zote tutahakikisha zinaonyweshwa live ili kuona kila kitu kinachoendelea ili tupate kuona kila kitu kinachoendelea,” alisema Mguto ambaye ni kiongozi wa Coastal Union.

4 COMMENTS:

  1. Hii ndio inaitwa kichwa Cha mwenda wazimu bingwa ameisha patikana tangu zamani.

    ReplyDelete
  2. Mlikua wapi watu wanapewa penati 2 msifunge hayo makamera yenu. Mshaona watu wamefanikiwa ndio mnakuja kujikosha

    ReplyDelete
    Replies
    1. HATA PENATI 5 KWENYE MCHEZO MMOJA INAWEZEKANA HAIJAKATAZWA MUHIMU ZIWE PENATI HALALI. ZILE 2 ZILIKUWA HALALI KABISA.

      Delete
  3. Kwani sheria zinakataza penalti mbili?Yondani kapigana mechi nä Biashara umesikia kelele?Kelele mnazo nyie vyura kwa sababu ya kuzoea kubebwa enzi za Malinzi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic