May 17, 2019


KIPA wa Simba anayeichezea Ndanda FC kwa mkopo, Said Mohamed ‘Nduda’ amesema yupo tayari kuitumikia Yanga msimu ujao.

Kauli hiyo aliitoa hivi karibuni mara baada ya aliyekuwa kipa wa Yanga, Beno Kakolanya kusitisha mkataba wa kuichezea timu hiyo na kuwa huru kusaini popote.

Kipa huyo, hivi sasa anaruhusiwa kufanya mazungumzo kwa ajili ya kuichezea timu nyingine itakayomhitaji kwa mujibu wa kanuni za soka kwa kuwa mkataba wake umesaliwa na mwezi mmoja pekee.

Nduda alisema yupo kuichezea Yanga kama wakihitaji huduma yake. “Ujue mimi soka ni kazi ambayo inaendesha maisha yangu ya kila siku, kitu cha kwanza ni maslahi yatakayoniwezesha nisaini mkataba kwenye timu itakayonihitaji kwenye msimu ujao wa ligi.

“Yanga ni timu yangu niliyowahi kuichezea, hivyo sitapata tabu kama nitarejea, nitakuwa kama ninarudi nyumbani kwani ni moja ya timu zilizonifikisha hapa nilipo katika maisha yangu ya soka baada ya Majimaji.

“Nitasaini mkataba wa kuichezea Yanga kama watakubali kunipa kile ninachokihitaji, kuhusu mipango ya kurejea Simba bado sijajua, mkataba wangu unakwenda ukingoni na hakuna mazungumzo yoyote na mabosi wa Simba,” alisema Nduda.

1 COMMENTS:

  1. Mimi nilifikiri kuwa Uongozi Mpya umeingia mambo yanaenda kuwa na "afueni" pale Yanga imekuwa tofauti....kwani wachezaji tegemeo wanauzwa....mechi za zikiendelea, sherehe za Michango zinasitishwa na kuahirishwa, Kocha anakimbia/kwenda nje kuuza mchezaji, ahadi hewa na michakato na uongo kila kukicha....sasa sijui wana nia ipi? Wanayanga hebu jibuni haya maswali kabla chombo "akijaenda mrama"....msipumbazwe, Simba wanafurahia hii hali yenu.....kumekuwa na jitihada za kuwapotosha na kuwahadaa na kuwaridhisha wakati chombo hakiendi sawa.....msilale Yanga amkeni....."wanawapetipeti" kwa lugha za kuwalainisha mitandaoni....lakini ukweli ni kuwa hawana nia ya kuona Yanga inaimarika.....Fanyeni uchunguzi kwani kila maoni ya kupata wachezaji bora, benchi bora la ufundi na mambo mengine ya kuimarisha timu yanapotolewa utaona wanasema msajilini mchezaji fulani (wa bei ya chini kutoka hapa Tanzania tena mwenye kiwango cha kawaida, na ambae anatoka Simba au hata timu nyingine hali kiwango chake hata Simba hafai) ....Yanga kama mnataka maendeleo msikubali kuyumbishwa takeni na himizeni yaliyo juu hasa nikimaanisha usajili wa wachezaji level juu). Pili suala la kubadilisha mfumo wa uendeshaji lazima wawekezaji waanze kutafutwa ndani ya miezi 3....
    Kuna upotoshwaji na nia ya kutaka kuwatoa Yanga "nje ya reli/mstari"....wanachama na mashabiki amkeni sasa hivi mkihoji hivi vitu kabla vitu havijaharibika.....Uongozi huu lazima hukidhi matakwa ya wanayanga kuwa na timu bora....lakini dalili ya mvua ni mawingu.....nina maana kila mtu alifikiri Yanga itafanya usajili bora na kuanza kusuka kikosi bora haraka, lakini hali si hivyo....wanauza wachezaji tegemeo (makambo, nasikia tetesi fei toto yuko njiani pia) bila kureplace hii si dalili nzuri

    Mwisho wa Maoni...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic