May 17, 2019


VIONGOZI wapya wa Yanga, juzi Jumatano walikutana na wachezaji wa timu hiyo na kuzungumza nao kwa takribani saa moja na ushee katika makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo maeneo ya Jangwani jijini Dar.

Katika mazungumzo yao hayo, kubwa ilikuwa ni kujadili juu ya malipo yao ya mishahara ambayo walikuwa wakidai kwa muda wa miezi minne na mambo mengine binafsi.

Wachezaji wa Yanga wamekuwa na madai ya muda mrefu ya mishahara pamoja na wengine wakidai kumaliziwa fedha zao za usajili na hii ni kutokana na hali ambayo klabu hiyo imekuwa ikipitia kwa sasa.

Katika kikao hicho ambacho Spoti Xtra lilikishuhudia Jangwani, kamati mpya ya utendaji pamoja na wachezaji walipata wasaha wa kukutana na kubadilishana mawazo ikiwemo kufahamiana.

Licha ya kwamba Mshindo Msolla hakutaka kusema kilichozungumzwa ndani, lakini Spoti Xtra limedokezwa kwamba wachezaji wameahidiwa kulipwa stahiki zao kabla ya msimu kumalizika na hata wanaoachwa wataambiwa mapema.

Taarifa ambazo Spoti Xtra imezipata ndani ya Yanga zimesema kuwa, katika kikao hicho ambacho kimedumu zaidi ya saa moja na nusu, wachezaji waliridhia na wameahidi kupambana kwenye mechi mbili zilizobaki.

Baadhi ya nyota ambao walikuwa kwenye kikao hicho ni pamoja na nahodha Ibrahim Ajibu, Amissi Tambwe, Thabaan Kamusoko, Juma Abdul, Juma Mahadhi, Paul Godfrey ‘Boxer’ Said Makapu na wengine ambao walikuwa ndani muda mwingi wakijadiliana mambo mazito.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic