OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa hakuna namna nyingine ya kufanya leo kwa kikosi cha Simba mbele ya Ndanda Uwanja wa Uhuru zaidi ya kubeba pointi tatu, tunajua ni timu nzuri na tunawaheshimu.
Mchezo wa leo utakuwa wa mzunguko wa pili kwani wa kwanza walicheza uwanja wa Nangwanda Sijaona na wote waligawana pointi moja moja.
"Tunatupa karata muhimu leo dhidi ya Ndanda FC,tukifanikiwa kupata Points tatu maana yake ni hii ,tutakuwa tumeshikilia kombe kwa mkono mmoja.
"Njooni tuchagize kibingwa, njooni mashabiki wetu wajivuni , mnaotufanya tutembee vidari mbele, kiporo cha korosho kinachacha kwani? Hakuna mchezo wa kupoteza kwa sasa wachezaji wanamorali kubwa," amesema Manara.
Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na poiti 85 na imebakiwa na michezo minne huku Ndanda ipo nafasi ya saba ikiwa na pointi 47 na imebakiwa na michezo mitatu.
0 COMMENTS:
Post a Comment