HII SASA NI SIFA, WATATU TOKA SIMBA WATAJWA KUTUA JANGWANI
Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Fredrick Mwakalebela amesema wako kwenye mpango wa kuwasajili wachezaji watatu wa klabu ya Simba, Aishi Manula, Jonas Mkude pamoja na Clatous Chama. Imeelezwa.
Taarifa hiyo imeripoti kuwa Mwakalebela kwa kujiamini alisema wachezaji hao watatu wanaweza kuonekana wakivaa jezi za Yanga msimu ujao.
“Jonas Mkude tunajua kwamba anataka kwenda nje kucheza soka la kulipwa, hataki tena kuongeza mkataba Simba, lakini sisi tunataka kumbakiza”
“Manula (Aishi) naye mkataba wake umefikia ukingoni na tumeanza naye mazungumzo, japo Simba nao wamefanya naye mazungumzo lakini hawajafikia mwafaka kwa sababu anataka wampe milioni 150, Simba wamegoma”
“Kwa upande wa Chama tunajua ana mkataba, lakini tukikubaliana tunawafuata Simba na kuvunja mkataba kwa sababu tunamhitaji na tuna amini tutalimaliza vizuri,".
Pesa zenu za viazi na nyanya mnaweza kuchukuwa wachezaji Simba???
ReplyDeleteYaan yanga ni viazi.umuchukue manula aende kushindia mihogo.hawajitambui bora mzee akikimali
ReplyDeleteHao wote wameshaongezewa miaka 2 mpaka 3 sasa wanasajiliwaje tena?
ReplyDeleteHalafu hata team haishiriki kombe lolote basi itakuwa hawana akili vizur
ReplyDeleteMkude, Haruna , Okwi, Chama na Manula wote wameshaongezwa mikataba
ReplyDeleteUnavocopy habar toka gazeti la Dimba .. Uwe unachanganya na zako. Simba na Yanga unajua kabisa kuuziana wachezaji ni kama ndoto.. Wanaweza kutaja ila wanao uwezo?? Hlo ndo swal la kujiuulza.. Team haijalpa mishahara miez mng wengne wakasusa hata kuitumikua team (Kakolanya). Wanasema wana bilion 1.5 but kocha anasema si kwel..
ReplyDeleteWakati mwingine unatuvunja moyo tunaotembea blog yako kla mda... N zaid ya madudu ... kumbuka hli s gazet kwamba watu wanunue ... but n blog ambayo inatakiwa itoe kitu special kiwe na ukwel angalau 56% tofaut na udak 🤔🤔... Ok nasubr kusoma Chama kaenda Yanga
ReplyDeleteJaman acheni fikra za kijinga wakati manila,boco na kapombe wanajiunga simba simba walikua mabingwa??kwaiyo swala la mchezaji kuhama no maslahi tu wala sishangai
ReplyDeleteWachezaji wote waliotajwa walishaongezewa mikataba, Na kwa bahati nzuri ni Blog hii hii kama sikosei ndiyo iliyoripoti taarifa hizo.
ReplyDeleteWanayanga wanataka vitendo wamechoka na ahadi na mipango.....sajilini wachezaji waonekane sio ahadi tupu na mipango na michakato!
ReplyDeleteHuyu kalewa kweli ivi chama au Manila aenda ya kipindi hichi kutafuta nn
ReplyDeleteNdio tuseme Yanga wanajivunia hela ya zungusha bakuli ya kuweza kuwavutia kina Manila. Jamaa wanajitutumuwa ka vile Bata mzinga
ReplyDelete