May 6, 2019

YANGA Leo imeyaaga mashindano rasmi ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kukubali kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Lipuli mchezo uliochezwa uwanja wa Samora.

Lipuli iliyo chini ya Kocha Sele Matola ilitumia dakika 45 kuumaliza mchezo kwani walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao mawili hali iliyofanya kuwapa nguvu ya kurejea kipindi cha pili kulinda mabao yao hayo.

Dakika ya 29 Paul Nonga aliandika bao baada ya mlinda mlango wa Yanga Klaus Kindoki kutema mpira uliopigwa na mshambuliaji wa Lipuli, Miraji Athuman ukazama kabla ya dakika ya 39 mabeki tena kujichanganya na kumuachia Miraji Athuman kuandika bao la pili kwa Lipuli.

Jitihada za Lipuli kusawazisha mabao hayo kipindi cha pili ziligonga mwamba licha ya kuonesha nia ya kutafuta mabao ukuta wa Lipuli uliokuwa chini ya Ally Mtani ulizuia mashambulizi yote ya Yanga.

Makosa ya safu ya ulinzi wa Yanga iliyokuwa chini ya Abdallah Shaibu 'Ninja' yameigharimu Yanga na kupoteza mchezo wa leo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga kurejea Dar kujiandaa na  michezo yao ya Ligi ili kuendelea kwenye mbio za ubingwa ambao ushindani wake umezidi kuwa mkubwa kwa timu tatu za juu ambazo ni pamoja na Simba na Azam FC.

Fainali itawakutanisha Azam FC na Lipuli itakayochezwa uwanja wa Ilulu, Lindi na mshindi wa michuano hii ataiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa.

5 COMMENTS:

  1. Mtoe azam mbio za ubingwa hata ashinde gem zilizobski anafikisha 79 ambazo yanga ameshavuka

    ReplyDelete
  2. Mwinyi Zahera kaeleza kuwa objectif (malengo)ya Yanga ni katika ligi kuu ilikuwa ni kumaliza ligi katika namba 5 au 6 katika ligi kuu na sio kuwa chini ya namba kumi! Pia hawakuwa na lengo la kuchukua kombe la FA cup!
    Hatudanganyiki...Hii ni sawa na hadithi ile aliyekuwa anarukia ndizi mbivu...Aliposhindwa akasema sizitaki mbichi hivi...Sikuwa na nia ya kweli ya kupata zile ndizi.
    Ni Zahera yule yule aliyepeleka kikosi cha pili Zanzibar ili kikosi cha kwanza kijiandae vema na mechi za ligi na FA cup! Akakosa Mapinduzi cup, atakosa Ubingwa na chance ya kucheza na Sevella!Na ni Zahera huyu huyu ambaye wakati Simba INAANZA cheza viporo alikuwa anaongelea namna Yanga itakuwa bingwa..Amepoteza matumaini wiki hiƧ tu baada ya kuona viporo vyote so far isipokuwa cha Kagera vimekuwa havichachi! Huyu kocha ni bora kwa maneno...anaropoka, payuka na kubadilika badilika!Hongereni kwa kupata viongozi wapya!

    ReplyDelete
  3. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  4. Uongozi mpya wa Yanga utathmini maendeleo na kwanini timu haijafanikiwa....ingawa ni kweli kuwa huyo kocha amewasaidia lakini lazima kuwepo na kubadilishwa na kuliimarisha benchi zima la ufundi...msiridhike kwakuwa mnaongoza ligi na mmefikia nusu fainali ya FA. Ukweli ni kwamba timu ina mapungufu mengi sana....caliber ya wachezaji wa Yanga wengine hawakufaa kuwemo kwenye hii timu wengi wao viwango ni vya chini mno, na umri umesogea mno. Pia mwalimu wa viungo, kocha wa makipa, madaktari, mameneja na wachua misuli....bado ni wa level ya chini hawana tofauti na wa timu za Ndanda, Alliance nk....usajili na viwango vya professional players ni duni....ndio unaweza ukadai kuwa tatizo ni pesa lakini hata hivyo baadhi yao hata scouting was very poor, na hawakuwa fiti, kuporomoka kwa uchezaji wao na umri umesogea mno, wachezaji wengi wazawa pia kuna kushuka kwa viwango kama ilivyo kwa wageni......timu kama Lipuli siyo ya kuitoa Yanga....yaliyopita si ndwele sasa nyinyi yeboyebo mugange yajayo....USAJILI WA KIWANGO CHA JUU NA KULIIMARISHA BENCHI LA UFUNDI....Challenge ni kushawishi wachezaji waliopo ambao wameibeba timu kubaki kikosini....kwa kusaini mikataba mipya!....Kuhusu Uwezo wa Mwalimu Noeli Mwandila....sidhani kama unaridhisha....kila ambapo Mwalimu Zahera akiondoka kwenda kwenye timu ya Taifa Kongo....akirudi viwango vya wachezaji vinakuwa chini mno....physical fitness is very low!...lazima ili liangaliwe....madaktari pia wachezaji walio majeruhi Yanga huchukua muda mrefu kupona....nadhani kuna haja ya kuipa uwezo na vifaa vya kisasa idara ya utabibu....yako madhaifu mengi mfano mengine kama kutokuwepo kwa ubora wa kambi na viwanja vya mazoezi, na kadhalika lakini haya ndio ya msingi....sasa mengine yalichangiwa na uongozi dhaifu na uchumi kudorora sasa hivi au msimu ujao hilo lisiwe tena kisingizio!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic