MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Lionel Messi amefikisha mabao 600 baada ya kufunga mabao mawili kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool kwenye ushindi wao wa mabao 3-0 uwanja wa Nou Camp.
Muargentina huyo alibaki kwenye rekodi ya mabao 599 baada ya kufunga bao lake la kwanza dhidi ya Liverpool ila mpira wa faulo alioupiga kwa mtindo wa "Magnificent' lilimfanya afikishe mabao 600.
Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa hajashangazwa na bao la mwisho lililofungwa na Messi kutokana na mtindo alioutumia.
"Ilikuwa ngumu kuamini ila najua kwamba Messi ni mchezaji wa daraja la juu duniani, kwa namna alivyocheza na namna alivyofanya sijashangazwa, kwa muda huu, jamaa hazuiliki, ulikuwa ni mchezo mzuri na wenye ushindani," amesema Klopp.
0 COMMENTS:
Post a Comment