May 2, 2019



MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa kikosi chake kilicheza vizuri kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya kupoteza kwa kufungwa mabao 3-0 mbele ya Barcelona.

Mshambuliaji Luis Suarez alianza kuwapa maumivu wachezaji wa Liverpool kipindi cha kwanza kabla ya mshambuliaji Lionel Messi kufunga mabao mawili yalioizamisha Liverpool hivyo watakuwa na kazi ya kufanya Jumanne uwanja wa Anfield.

"Sina uhakika kama tutacheza vizuri zaidi, ila nina imani utakuwa mchezo mgumu na mzuri kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, sio kwa mwaka huu pekee bali hata mwaka uliopita pia.

"Niliwaambia vijana nimejivunia sana namna walivyocheza dhidi ya wapinzani wetu, walicheza mchezo mzuri na ni namna walivyofanya wamenifanya nitabasamu.
"Mwisho wa siku ni matokeo ambayo tumeyapokea kwa kufungwa mabao 3-0 kwenye mpira chochote kinaweza kutokea, hakuna ambaye amependa matokeo haya ila hakuna namna ya kufanya tumepoteza, nitatumia mchezo huu kuwaambia vijana kwamba mpira unachezwa namna hii," amesema.
Liverpool jana uwanja wa Nou Camp walikuwa mbele kwa umiliki wa mpira ambapo walikuwa wanaongoza kwa asilimia 57 na walicheza pasi 284 huku Barcelona wakicheza pasi 217 na mashuti manne walipiga langoni huku wapinzani wao wakipiga mashuti matatu yaliyolenga lango.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic