May 2, 2019

UONGOZI wa Simba umeamua kuibukia kwa kiungo wa Azam FC, Salum Aboubakar 'Sure Boy' kutokana na uwezo wake uliojificha kwenye miguu yake.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, kupitia ukurasa wake wa Istagram amesema kuwa kama angekuwa Kocha Mkuu wa timu ya Taifa angemuita ndani ya kikosi.

"Sure Boy ana nn ? Kuna mahali anakosea au mm ndio sijui mpira? kitu gani kinamtokea fundi huyu anaepiga pasi za mwisho za hatari kuliko kiungo yoyote nchini.

"Yeye ndio mido anaeamua team icheze vipi ktk ligi hii kando ya Haruna Niyonzima 
Salum Aboubakar 'Sure Boy' lau mimi ningekuwa kocha wa timu ya Taifa,sio tu ningemwita kwenye kikosi bali angekuwa anaanza katika first eleven ya Team (Kikosi cha kwanza).


"Emmanuel Amunike nakuomba usifunge milango kwa wachezaji, nenda umuangilie tena midfielder huyu bora na mwenye uzoefu wa kutosha," amemaliza Manara.

2 COMMENTS:

  1. Ndio maana hukua ,wewe unahis ukocha ni kuongea tu

    ReplyDelete
  2. Kabisa kabisa we Manara waswahili husema mtu akizaliwa kwenye pesa na yeye kumkuta na pesa si ajabu. Inashangaza sana kwanini salum Abubakari hakuwemo japo kwenye kikosi cha awali? Halafu Amunike alionekana akisema kuwa kaita wachezaji wengi kwa sababu ya mashindano ya CHAN pia. Inamaana hata kwa CHAN pia Sure boy hana uwezo? Sure boy ni kiungo mkomavu,Mtulivu pia na mjanja na unaweza kusema bila ya uoga ni miongoni mwa viungo wachache nchini wenye uwezo wa kuuchezea mpira na mpira ukachezeka. Kwa maana yakwamba anaujua mpira hasa,si vibaya kusema Sure aliujua mpira kabla hajazaliwa,lakini ndio hivyo tena. Siku ikitokea Magufuli kuteua wachezaji wake wa timu ya Taifa na kusema mimi nataka hawa ndio wacheze sidhani kama watanzania watashngaa.Ninacho kiamnini mimi Amunike anakosa washauri wazuri au tuseme anakosa watu wenye jicho la mwewe na sikio la paka katika kuona na kusikia mambo ya ufundi katika uteuzi na upangaji kwa wachezaji wa timu ya Stars. lakini wakati mwengine kuna vitu hatuhitaji hata jicho la kinyonga kujua mchezaji gani anafiti kwa ajili ya timu ya Taifa. Ila watu wakitoa maoni yao wanaonekana wajuaji,wakorofi wanaingilia kazi za watu? Kwa timu ya Taifa na sio timu ya TFF ni timu ya watanzania na kila Mtanzania ana haki kutoa maoni yake kuhusiana na jinsi anavyoona hali ya timu hiyo. Tunasikia tumu itaweka kambi Misri ila katika kundi letu kuna timu kama Kenya inatoka Africa Mashariki kitaalamu tulitakiwa kutafuta katika mechi za kujipima nguvu timu za ukanda huu kwanza wanaoshabiana na soka la Kenya mfano Uganda na Ethiopia. Kwa Wasenegali timu ya Mali ingekuwa timu nzuri ya kujipima nguvu. Kwa Algeria tayari inasemakana stars itacheza na Misri. Kuweka kambi sio big deal hata kidogo kuelekea Afrcon kwa Taifa stars. Kitu kilichokuwa big deal kwa Taifa stars ni kupata mechi za kutosha za kujipima nguvu kabla ya mashindano hayo ili kuwaongezea wachezaji match fitness na kulipa benchi la ufundi tasmini ya mapema kati ya wachezaji wetu na mataifa mengine. Ila kuweka kambi tu sioni akili ya kuweka kambi kwa muda mrefu kwa timu ya taifa iko wapi? Karibu wachezaji wote wa taifa stars watakuwa wanatoka kunako msimu mrefu wa ligi mbali mbali nchini na duniani,hawa wachezaji wapo fiti kinachohitajika ni kupata uzoefu wa mechi kubwa za kutosha za kimatifa za kujipima nguvu that's all.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic