May 6, 2019


KOCHA wa Lipuli, Seleman Matola amesema kuwa hamna njia yoyote itakayowafanya watimize lengo lao la kubeba kombe la Shirikisho zaidi ya kuwafunga Yanga na kutinga hatua ya fainali.
Akizungumza na Saleh Jembe, Matola amesema kuwa wanaitambua vizuri timu ya Yanga na mbinu zake zote anazitambua hivyo haoni kitakachomzuia ashindwe kuifunga na kutinga hatua ya fainali.
"Mpaka sasa tayari tumecheza mechi nyingi kufikia hapa, sasa kama mechi zote nimepata matokeo chanya nitashindwaje kupata matokeo mbele ya Yanga tena uwanja wa nyumbani? Itakuwa ajabu kwa kuwa timu ina malengo.
"Ninaiheshimu Yanga ni timu nzuri na ina mwalimu mzuri ila linapokuja suala la matokeo ni lazima tuwashangaze, tumedhamiria kutinga hatua ya fainali na kurejea na kombe hapa nyumbani, mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti," amesema Matola.
Mshindi wa mchezo wa leo atamenyana na Azam FC, Lindi uwanja wa Ilulu, mchezo wa hatua ya fainali ambapo bingwa ataiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa ya kombe la Shirikisho Afrika.

1 COMMENTS:

  1. Uongozi utathmini maendeleo na kwanini timu haijafanikiwa....ingawa ni kweli kuwa huyo kocha amewasaidia lakini lazima kuwepo na kubadilishwa na kuliimarisha benchi zima la ufundi...msiridhike kwakuwa mnaongoza ligi na mmefikia nusu fainali ya FA. Ukweli ni kwamba timu ina mapungufu mengi sana....caliber ya wachezaji wa Yanga wengine hawakufaa kuwemo kwenye hii timu wengi wao viwango ni vya chini mno, na umri umesogea mno. Pia mwalimu wa viungo, kocha wa makipa, madaktari, mameneja na wachua misuli....bado ni wa level ya chini hawana tofauti na wa timu za Ndanda, Alliance nk....usajili na viwango vya professional players ni duni....ndio unaweza ukadai kuwa tatizo ni pesa lakini hata hivyo baadhi yao hata scouting was very poor, na hawakuwa fiti, kuporomoka kwa uchezaji wao na umri umesogea mno, wachezaji wengi wazawa pia kuna kushuka kwa viwango kama ilivyo kwa wageni......timu kama Lipuli siyo ya kuitoa Yanga....yaliyopita si ndwele sasa tugange yajayo....USAJILI WA KIWANGO CHA JUU NA KULIIMARISHA BENCHI LA UFUNDI....Challenge ni kushawishi wachezaji waliopo ambao wameibeba timu kubaki kikosini....kwa kusaini mikataba mipya!....Kuhusu Uwezo wa Mwalimu Noeli Mwandila....sidhani kama unaridhisha....kila ambapo Mwalimu Zahera akiondoka kwenda kwenye timu ya Taifa Kongo....akirudi viwango vya wachezaji vinakuwa chini mno....physical fitness is very low!...lazima ili liangaliwe....madaktari pia wachezaji walio majeruhi Yanga huchukua muda mrefu kupona....nadhani kuna haja ya kuipa uwezo na vifaa vya kisasa idara ya utabibu....yako madhaifu mengi mfano mengine kama kutokuwepo kwa ubora wa kambi na viwanja vya mazoezi, na kadhalika lakini haya ndio ya msingi....sasa mengine yalichangiwa na uongozi dhaifu na uchumi kudorora sasa hivi au msimu ujao hilo lisiwe tena kisingizio!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic