May 6, 2019


KATIKA kuongeza morali ya wachezaji ili wawafunge wapinzani wao Yanga, uongozi wa Lipuli FC umewaahidi wachezaji wao shilingi milioni 15 kama wakifanikiwa kuwafunga. Yanga na Lipuli zinatarajiwa kuvaana leo Jumatatu katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho utakaopigwa kwenye Uwanja wa Samora.

Katika mchezo huo, Lipuli wataingia uwanjani wakiwa na rekodi ya kuwafunga Yanga katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Samora, Iringa.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo tumezipata, wachezaji hao wameahidiwa kupewa fedha hizo mara baada ya mchezo huo kumalizika kwa wao kushinda.

Mtoa taarifa huyo alisema, wachezaji wameahidi kupambana kufa au kupona kuhakikisha wanashinda mchezo huo unaotarajiwa kujaa upinzani mkubwa kutokana na maandalizi waliyoyapata kutoka kwa kocha wao, Selemani Matola.

“Tumeona umuhimu wa mchezo huu dhidi ya Yanga, hivyo ni lazima tushinde ili twende kucheza fainali na baadaye tuchukue kombe.
“Katika kuongeza hamasa ya wachezaji, tumeona tuwaahidi kiasi kidogo ambacho kwao kitakuwa kikubwa ili tufanikishe malengo yetu.

“Haitakuwa kazi nyepesi tunafahamu kwani Yanga nao wamepania mchezo huu kupata matokeo mazuri ya ushindi ambayo na sisi tunayahitaji,” alisema mtoa taarifa huyo.

Alipotafutwa Matola kuzungumzia hilo, alisema: “Bado sijazipata taarifa hizo rasmi, lakini hilo suala la ahadi linakuwepo mara kwa mara kwa viongozi wetu na uzuri ni kuwa wachezaji wangu wanajua umuhimu wa kila mechi.

“Kikubwa tunahitaji ushindi pekee katika mchezo wetu na Yanga, maandalizi yamekamilika na tunachosubiria ni mchezo huo.”

CHANZO: CHAMPIONI

5 COMMENTS:

  1. Ningependa zaidi Yanga kusonga mbele ila kwakweli hivi vihunzi viwili vya Simba B vya lipuli na Azam akivuka Yanga basi ana haki ya kutembea kifua mbele.

    ReplyDelete
  2. KUNA MASWALI NAJIULIZA:-
    1.LIPULI AKICHUKUA UBINGWA SI ATAENDA KUTUTIA AIBU KIMATAIFA
    2.KWA NINI MCHEZO UCHEZWE IRINGA KWENYE KIWANJA KIBOVU
    3.JE INAWEZEKANA KUA TFF INATAKA TUWAKILISHWE NA TIMU DHAIFU
    4.KWA NINI KARIBU MECHI ZOTE ZA YANGA KOMBE LA FA ZIMECHEZWA NJE YA DAR

    ReplyDelete
  3. Masikini yanga, kila siku marefa watuonea. Nina Hakika hata ubingwa itakuwa maonevu na stayepewa ni Simba

    ReplyDelete
  4. LIPULI SI DHAIFU SIMBA NA HANS POPE WATAWAPA WACHEZAJI WA KIMATAIFA

    ReplyDelete
  5. Uongozi utathmini maendeleo na kwanini timu haijafanikiwa....ingawa ni kweli kuwa huyo kocha amewasaidia lakini lazima kuwepo na kubadilishwa na kuliimarisha benchi zima la ufundi...msiridhike kwakuwa mnaongoza ligi na mmefikia nusu fainali ya FA. Ukweli ni kwamba timu ina mapungufu mengi sana....caliber ya wachezaji wa Yanga wengine hawakufaa kuwemo kwenye hii timu wengi wao viwango ni vya chini mno, na umri umesogea mno. Pia mwalimu wa viungo, kocha wa makipa, madaktari, mameneja na wachua misuli....bado ni wa level ya chini hawana tofauti na wa timu za Ndanda, Alliance nk....usajili na viwango vya professional players ni duni....ndio unaweza ukadai kuwa tatizo ni pesa lakini hata hivyo baadhi yao hata scouting was very poor, na hawakuwa fiti, kuporomoka kwa uchezaji wao na umri umesogea mno, wachezaji wengi wazawa pia kuna kushuka kwa viwango kama ilivyo kwa wageni......timu kama Lipuli siyo ya kuitoa Yanga....yaliyopita si ndwele sasa tugange yajayo....USAJILI WA KIWANGO CHA JUU NA KULIIMARISHA BENCHI LA UFUNDI....Challenge ni kushawishi wachezaji waliopo ambao wameibeba timu kubaki kikosini....kwa kusaini mikataba mipya!....Kuhusu Uwezo wa Mwalimu Noeli Mwandila....sidhani kama unaridhisha....kila ambapo Mwalimu Zahera akiondoka kwenda kwenye timu ya Taifa Kongo....akirudi viwango vya wachezaji vinakuwa chini mno....physical fitness is very low!...lazima ili liangaliwe....madaktari pia wachezaji walio majeruhi Yanga huchukua muda mrefu kupona....nadhani kuna haja ya kuipa uwezo na vifaa vya kisasa idara ya utabibu....yako madhaifu mengi mfano mengine kama kutokuwepo kwa ubora wa kambi na viwanja vya mazoezi, na kadhalika lakini haya ndio ya msingi....sasa mengine yalichangiwa na uongozi dhaifu na uchumi kudorora sasa hivi au msimu ujao hilo lisiwe tena kisingizio!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic