May 2, 2019



UONGOZI wa Simba umesema kuwa kwa sasa hesabu zao kubwa ni kupata matokeo kwenye mechi zao zote zilizobaki licha ya ushindani mkubwa wanaoupata kwa sasa kwenye ligi.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mratibu wa Simba, Abas Abdalah amesema kuwa kikosi kipo imara na wanapambana kupata matokeo.

"Kwa sasa tupo vizuri na tuna kazi ngumu ya kufanya kwenye ligi kutokana na malengo ambayo tumejiwekea, ligi ni ngumu hilo lipo wazi ila tunapambana katika michezo yetu iliyobaki.

"Hakuna mchezaji ambaye ni mgonjwa kwetu zaidi ya Shomari Kapombe ambaye naye ameanza mazoezi wengine wote wapo fiti kwa ajili ya kupambana," amesema.

Simba kesho inashuka uwanjani kumenyana na Mbeya City mchezo utakaochezwa uwanja wa Sokoine.

2 COMMENTS:

  1. Mechi mbili za Mbeya ni mechi za ubingwa.siku zote Mbeya city na Tanzania prison mechi zao huwa hazi tabiriki hasa zikiwa kwao. Kujua kiasi gani Simba ana ubavu wa kuutetea ubingwa wake basi ni hizi mechi mbili za Mbeya.

    ReplyDelete
  2. Simba tatizo beki pia kwani kama washambuliaji wa JKT wangekuwa makini kidogo basi hii leo tungekuwa tunazungumzia habari nyengine kabisa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic