May 18, 2019


USHINDI wa mabao 6-0 Manchester City dhidi ya Watford kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la FA uliochezwa uwanja wa Wembley umetosha kuipa City ubingwa huo.

City wamevunja rekodi kubwa ambayo imedumu kwa miaka 116 rekodi ambayo Sir Alex Ferguson alisema itakuwa ngumu kuvunjwa ya kwenye fainali.
Mabao ya City yamefungwa na  David Silva aliyefungua pazia dakika ya 26 Raheem Sterling alitupia hat trick dakika ya 39, 81 na 87, mabao mengine yamefungwa na De Bryne dk ya 61 pamoja na Jesus dk ya 68.
Hili linakuwa ni kombe la nne kubeba kwa Manchester City msimu huu baada ya lile la Ligi Kuu ambapo ukijumlisha yote ambayo ametwaa kocha Pep Guardiola yanafika manne pamoja na lile la Carabao bila kusahau ngao ya Jamii.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic