May 18, 2019


VIONGOZI wa Yanga leo wamekutana kwenye hafla maalumu ya Ifttar iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwapongeza wachezaji kwa kupambana kwenye Ligi Kuu Bara licha ya kupitia kwenye kipindi kigumu iliyofanyika kwenye hotel ya Serena.

Yanga  kwa sasa ipo nafasi ya pili imejikusanyia pointi 82 na imebakiwa na michezo miwili mkononi kwa ajili ya kumaliza michezo yake ya msimu huu.

Halfa hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Yanga, wachezaji pamoja na mashabiki wa kikosi hicho huku kocha Mkuu, Mwinyi Zahera pamoja na mshambuliaji Heritier Makambo wakiwa ni sehemu ya waliohudhuria hafla hiyo.

Pia lile zoezi ambalo lilitarajiwa kufanyika leo kwa ajili ya kuchangia timu hiyo limesongezwa mbele mpaka Juni 15 mwaka huu, ukumbi wa Diamond Jubilee.

1 COMMENTS:

  1. Wanayanga wanataka vitendo wamechoka na ahadi na mipango.....sajilini wachezaji waonekane sio ahadi tupu na mipango na michakato!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic