May 18, 2019


IMEELEZWA kuwa baada ya wachezaji wa Simba jana  pamoja na benchi la ufundi kuonana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Simba, Mohammed Dewji, 'Mo' wameahidiwa kupewa zawadi ya shilingi milioni tano kwa kila mmoja endapo watatwaa kombe la ligi kuu.

Habari za ndani zimeeleza kwamba Mo amewaambia wachezaji kwamba kwa sasa wanapaswa wapambane kwenye michezo yao minne iliyobaki ili kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara utakaowapa nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo ikiwa na pointi 85 imebakiwa na michezo minne ili kumaliza michezo ya ligi msimu huu, huku wapinzani wao Yanga wakiwa nafasi ya pili na wana pointi 82 wamecheza michezo 36 wamebakiwa na michezo miwili mkononi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic