PEP Guardiola, Meneja wa Manchester City amesema kuwa mashabiki wa kikosi hicho wanaheshimu kile ambacho kinafanywa na wachezaji wake kwa sasa, hivyo leo hata kama watashindwa kupata matokeo kwenye fainali ya FA mbele ya Watford uwanja wa Wembley itakuwa ni kawaida.
"Watu hawajali kuhusu kushindwa kwetu, iwe ni Italia ama Hispania kila mahali tunaona fahari kuwa na mashabiki ambao wanakubali kile ambacho tumefanya. Ninahisi namna mashabiki wetu wanavyofurahi wakiwa mtaani, namna wanavyotuma ujumbe kwetu kutoka sehemu mbalimbali.
"Bado Manchester City inapambana na historia ili kuweza kufika hatua kama ilivyo Liverpool na Manchester United kwa namna zinavyotazamwa.
"Liverpool imepita miaka 29 bila ya kushinda Ligi Kuu ya England, ni kawaida watu bado wana imani ya kushinda mwishoni, kama Liverpool ingeshinda taji msimu huu yangekuwa ni mafanikio makubwa kwao ila kwa kuwa tumeshinda sisi basi ni mafanikio pia.
"Nadhani tumefanya maajabu kwa muda wa misimu miwili, lakini bado hatujafikia ubora ambao tunauhitaji, siwezi kusema kwamba nina kipindi bora kama ilivyokuwa kwa Sir Alex Ferguson msimu akiwa United ama Bob Paisley mwaka 1980 akiwa Liverpool.
" Mfano namna Liverpool na Manchester United zilivyo na umuhimu kwenye mitandao, habari ya kwanza Jumatatu iliyopita ilikuwa inazungumzia suala la Paul Pogba na mashabiki wa Manchester United uwanja wa Old Trafford na sio mimi ambaye nimeshinda taji la Ligi Kuu England, haina maana kwamba hatustahili ila ni umuhimu, bado hatuwezi kufanishwa nao hasa kwenye maamuzi," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment