May 18, 2019


MARCUS Rashford (21) mshambuliaji wa timu ya Manchester United amewagomea mabosi hao kuanza mazungumzo mapema kwa ajili ya kusaini mkataba mpya kwa ajili ya msimu ujao akiwa chini ya Meneja Ole Gunnar Solskjaer.
Rashford kwa sasa anajukumu la kufanya maamuzi kuhusu kujiunga na kikosi hicho msimu ujao ama kuangalia maisha mengine akiwa nje ya Manchester United.
Klabu ya Manchester United inahitaji huduma ya mshambuliaji huyo ambaye anachezea timu yake ya Taifa ya England wamejipanga kumpa dili kwa ajili ya misimu miwili ijayo.
Kwa mujibu wa The Sun, Rashford ameuambia uongozi wa klabu hiyo kwamba hana mahitaji ya kuongea na klabu hiyo kutokana na matamanio yake aliyonayo hapo baadaye.

Imeripotiwa kwamba Rashford amekuwa akilalamika juu ya imani yake kwa meneja Solskjaer akiamini kwamba uwezo wake umeshuka ghafla hali iliyofanya washindwe kutinga nne bora kwenye Ligi Kuu England na kukosa nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya kitu alichokuwa akikipigia hesabu muda mrefu.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic