May 6, 2019


MSHAMBULIAJI nyota wa Serengeti Boys, Kelvin John (Mbappe), amesema hakulala kabisa siku aliyoitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars, kutokana na watu wengi kumtafuta.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike, amemuita Mbappe kwenye kikosi cha wachezaji 39 wanaounda kikosi kinachojiandaa na mashindano ya Afcon, pamoja na Chan.

Mbappe alisema kuwa alikutana na wakati mgumu baada ya kuitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars, kwa kuwa watu wengi walikuwa wanampigia simu huku WhatsApp yake ikipokea meseji zaidi ya 200 kwa muda mfupi.

“Sikulala kabisa, simu zilikuwa nyingi sana, inatoka hii inaingia hii, WhatsApp yangu ilipokea meseji zaidi ya 200 kwa wakati mmoja, mwisho wa siku nikaamua kuizima simu kabisa ili nipate nafasi ya kulala,” alisema Mbappe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic