May 6, 2019


Alichokisema Jonas Tiboroha baada ya kushindwa kwa kura katika kugombea nafasi ya Uenyekiti Yanga

Yanga oyeeeeee!! Daima Mbele Nyuma Mwiko.

Napenda nitoe shukrani zangu kwa kamati ya uchaguzi, pili nawashukuru wapiga kura wote hakika wana Yanga mmeongea kwa sauti kubwa sana.

Hatimaye tumempata mwenyekiti, kama mgombea nampongeza sana mwenyekiti na pia namtakia kila la heri katika shughuli yake inayokuja, sio shughuli ndogo ila nna imani kubwa juu yake anaweza kutupeleka kwenye nchi ya ahadi.

Lakini mimi kama mwana Yanga nilishamtumia ujumbe wa pongezi ndugu mwenyekiti kwa kuwa nilishapata matokeo mapema kidogo!

Nimemwambia kabisa mimi kama mwana Yanga nipo tayari kumsaidia pale anapoona nafaa na kunihitaji.

Mwisho kabisa nawapongeza wale watu 60 walionipigia kura kwa maana kura zao zimewezesha kupatikana mshindi, ni muda sasa kuvunja kambi na utimu kuanzia sasa wote ni timu Msolla, Ahsanteni sana"

Na Jonas Tiboroha.

2 COMMENTS:

  1. ameongea kwa hekima sana na kuonesha ukomavu wa kiuongozi

    ReplyDelete
  2. Hongela Sana ndugu tiboroha kwakuwa ww mshabiki mkubwa Wa YANGA team ya wananchi na najua uligombea uwenyekiti kwakuwa ilizjua shida zetu hakika mungu akupe moyo huohuo wakupendana ili nao viongoz wengne wajifunze kutoka kwako asante Sana mwenyekiti wetu mpya ndugu msolla ninaamini ataifiksha team ya wananchi pale tunapotaka inshaaaalaaaah

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic