May 20, 2019


AZAM FC imefunga mabao 50 mpaka sasa katika michezo yake 36 idadi hiyo ni sawa na mabao waliyofunga washambuliaji watatu tu wa Simba ambao ni Emmanuel Okwi, John Bocco na Meddie Kagere.

Washambuliaji hao wanaounda utatu maridhawa, wanaweza kuongeza idadi hiyo ya mabao kutokana na kuwa na michezo minne kabla ya kumalizika kwa msimu huu kwenye ligi kuu.

Kagere ambaye ni kinara wa mabao kwenye ligi kwa sasa, amefunga mabao 22, huku Okwi na Bocco kila mmoja akifunga mabao 15. Azam FC ambayo inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi, hadi sasa imefunga jumla ya mabao 50, huku ikiruhusu kufungwa mabao 21.

Hata hivyo washambuliaji hao wameandika historia na rekodi kwa misimu mitano ya hivi karibuni kwani hakuna pacha hatari ambayo imefunga mabao 50.

Msimu wa 2015/16, pacha ya Yanga iliyokuwa na Amissi Tambwe, Simon Msuva na Donald Ngoma iliyofunga mabao 46. Simba mpaka sasa katika mechi zake 34, imefunga jumla ya mabao 72 na kuvunja rekodi ya Yanga ya mabao 70 ya msimu wa 2015/16.

Mpaka sasa kwenye msimamo wa wafungaji Kagere ndiye anayeongoza kwa mabao 20 huku Okwi na Bocco kila mmoja kasaliwa na bao moja kumfikia mshambuliaji wa Yanga Heritier Makambo mwenye mabao 16.

Kutokana na kasi hiyo, Kocha wa Simba, Patrick Aussems alisema kuwa, aliiandaa safu yake ya ushambuliaji tangu mwanzoni mwa msimu hivyo alitarajia kupata matokeo mazuri kwa wachezaji wake hao kwa kuwa wana viwango vizuri.

“Idadi ya mabao waliyoyafunga Okwi, Kagere na Bocco sio sapraizi kwangu, nilikiandaa kikosi changu tangu mwanzoni mwa msimu na nilikuwa natarajia matokeo haya ya kufunga mabao mengi.

“Ni wachezaji wazuri na wamekuwa wakipata nafasi nyingi za kufunga, wamekuwa wakishirikiana vizuri, walichokifanya wanastahili pongezi kwa kuwa ni kitu nilichokitarajia,” alisema Aussems ambaye bado Simba haijampa mkataba mpya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic