ZAHERA ATAJA SABABU ZA KUMPIGA CHINI HAJI MWINYI
KABLA ya kucheza na Azam FC, juzi Jumatatu, beki Haji Mwinyi alikuwa na uhakika mkubwa wa kuwepo katika mechi hiyo lakini dakika za mwisho, kocha wake Mwinyi Zahera akaamua kumchomoa na kumuondoa kwenye listi ya wachezaji wake ambao atawatumia kisha nafasi yake kumpa mtu mwingine.
Kocha huyo amesema kuwa alimuondoa beki huyo kwa kuwa alihitaji mchezaji anayeweza kucheza safu ya ulinzi na winga kwa wakati mmoja ndiyo maana akampa nafasi hiyo Jaff ary Mohammed ‘Rasta’ ambaye aliingia katika mechi hiyo akichukua nafasi ya Gadiel Michael.
Yanga juzi Jumatatu ilikuwa mgeni wa Azam FC katika mechi ya ligi ambayo ilipigwa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar na kupata ushindi wa bao 1-0.
“Huyu Jaffary kwenye mechi hii wala hakuwa sehemu ya kikosi ambacho kilikuwa kambini.
Nilikuwa na Mwinyi Haji ambaye yeye ndiye alitakiwa kucheza lakini dakika za mwisho nikaona nimuondoe kisha nikawaambia viongozi wampigie Jaff ary aje kuungana na wenzake.
“Nilitaka mchezaji ambaye ningeweza kumtumia kama beki lakini pia winga, hapo ndipo nilipompa nafasi yeye,” alisema Zahera.
0 COMMENTS:
Post a Comment