May 18, 2019


1. Mchezaji Emmanuel Okwi ameongeza mkataba wa miaka mitatu kuendelea kuitumikia klabu ya Simba SC. Okwi alikua anahusishwa kuondoka ndani ya miamba hao mwishoni mwa msimu huu.

2. Clotous Chota Chama yeye ameongeza mkataba wa miaka mitatu ya kuendelea kuitumikia klabu ya Simba.

3. Baada ya Azam FC kutikisa kiberiti ili ipate huduma ya Nahodha wa klabu ya Simba, John Rafael Bocco, hatimaye amesaini mkataba miaka miwili kuendelea kuitumikia klabu ya Simba SC.

4. Mnyarwanda Haruna Fadhili Hakizimana Niyonzima na yeye ameongeza kandarasi ya miaka miwili kuendelea kuitumikia Simba.

5. Kiungo Fundi Jonas Gerald Mkude baada ya kuhusishwa kuwa ataachana na kikosi cha mabingwa watetezi hao, pia amesaini Kandarasi ya miaka miwili kuitumikia klabu ya Simba SC

6. Golikipa Aishi Salum Manula amesaini kandarasi ya miaka miwili

Imeelezwa....

9 COMMENTS:

  1. Kapombe, Nyoni na wengineo hayanekani majina Yao huenda ikawa katika list ya baadae

    ReplyDelete
  2. Safi sana
    Ni hatua muhimu sana kuelekea mashindano makubwa kwa msimu ujao.

    ReplyDelete
  3. wenye umri mdogo miaka 2 wazee miaka 3

    ReplyDelete
  4. GYAN Jamani msimuache plz Ni muhimu sana GYAN

    ReplyDelete
  5. Safi kabisa wachezaji wazoefu ni dawa. Barcelona si wapumbavu kuona bado wanaendelea kuhitaji huduma za akina Pique na wengine wengi wazoefu. Kwa upande mwngine simba kocha na benchi lake la ufundi ndio wenye maamuzi ya mwisho kuhusu mchezaji gani anafaa lakini kuna mambo kocha wa Simba na benchi lake la ufundi wanapaswa kushauriwa kwa manufaa ya timu.Nicholas Gayan raia wa Ghana aliletwa Simba kama fowadi chipukizi anaenyanyukia kwa kasi huko kwao Ghana. Kwa bahati mbaya alipofika Tanzania mambo hayakuwa mazuri kwake na hata yeye mwenyewe alishakata tamaa na alishakuwa na maamuzi ya kurudi kwao lakini ujio wa Masoudi Djuma aliekuwa kocha msaidizi wa Simba aliona kitu kwa Gayani na kuamua kumueka sawa kiakili kitu ambacho alifanikiwa ila Gayani akabadilishiwa majukumu ya kazi uwanjani badala ya fowadi akarejeshwa kucheza beki mbili. Gayani kutoka senta foward asilia kwenda kucheza beki mbili lakini bado anaonekana kuitendea haki beki kuliko mabeki wengi asilia wa pembeni nchini. Sasa tatizo linaloonekana pale simba kwa Gayani ni kama vile Simba wao wenyewe hawataki kufaidika zaidi na kazi itakayokuwa bora zaidi kutoka kwa Gayani. Kwangu mimi Gayani ameshaiva na ni wakati muafaka wa kumsogeza kucheza nafasi za mbele alikokuzoea na nnaimani anaweza kufanya vizuri zaidi ya baadhi ya wachezaji wa mbele wa Simba. Wakati tayari Gayani ameshakuwa na mentality ya kucheza kama beki atakapocbeza fowadi haitakuwa taabu kwake kurudi kusaidia ulinzi timu inaposhambuliwa na ni nadra sana kupata fowadi waliokuwa wepesi sana kurudi nyuma kuja kusaidia ulinzi. Simba kweli wana tatizo la beki mbili ila wakati wa usajili unakaribia ni wakati muafaka kutafuta beki mbili wa ukweli kusaidiana na Kapombe au waendelee na zana kulibali. Na nisingeafiki kwa Simba kuachana na Gayani. Licha ya kocha wa Simba kusema kuwa hajaridhishwa na viwango vya wachezaji wazawa mimi nnaamini wachezaji wapo na ni vyema wakaongezwa japo wazawa wawili wenye uchu wa mafanikio. Na kama kweli Simba wapo serious na kutaka kuiimarisha Simba ili kuja kuwa ya ushindani zaidi mwakani basi wanatakiwa kuachana na Pascal Wawa,Juuko Murishdi na Asante kwasi na kutafuta wabadala wao watakaokuwa bora zaidi tena haraka bila ya kumumunya maamuzi. Wawa sie yule aliekuwa wa Azam ingawaje anajikaza ila hufanya makosa mengi kama beki wa kati na Simba wanaweza kumuajiri kama kocha wa mabeki kama wataafikiana nae. Juuko ni beki mzuri hakuna ubishi ila kwa kipindi kirefu sasa licha ya Simba kumstaamilia lakini hana ufanisi unaotoshezeleka pale simba na ni bora kutafuta beki muafaka na kama kuna wasiwasi sijui atakwenda Yanga basi ni bora aende la msingi ni kutafuta beki atakae kuwa bora zaidi yake. Asante kwasi ni beki mzuri tena sana ila anaonekana hayuko fiti kuna kitu kinamsumbua labda kasumba yakuwa anarogwa. Ila ni vizuri kuachana nae na nafasi yake kuzibwa na mchezaji wa kigeni mwenye tija zaidi.Nnaimani wahusika wanafuatilia maoni ya wadau kwani lengo kubwa kujenga Simba iliyobora zaidi na kwa kuanzia ni vyema kutathmini kwa kina mapungufu na uwezo wa Wachezaji waliokuwepo ndani ya Simba ya sasa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yes niko kweli ulichokizungumza

      Delete
    2. Simba inataka kuongeza wachezaji 4 wa kigeni. Je huoni ni lazima wachezaji 4 wa kigeni wapunguzwe? Bila hivyo hatuwezi kuongeza mchezaji

      Delete
  6. Uko sawa kabisa mkuu, Gyan na kotei sio wa kuachwa.Kuimarisha ulinzi.. Wawa, Murshid na kwasi wengepisha visiki vingine wenye ubunifu na akili kama za Nyoni.

    ReplyDelete
  7. Sure! Nicola Gyan na James Kotei waongezwe mikataba!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic