May 21, 2019

BAADA ya uongozi wa Singida United kupitia kwa Katibu, Festo Sanga kusema kwamba uwanja wa Namfua sio sehemu salama kwa Simba kutangaziwa ubingwa kwa kuwa wamejipanga kushinda, Ofisa Habari wa Simba Haji Manara amesema rekodi zinawabeba kwenye uwanja huo.

Manara amesema kuwa msimu uliopita wakati wanaifuata Singida, walitangazwa kuwa mabingwa baada ya Yanga kupoteza kwa kufungwa mabao 2-0 mbele ya Prisons hivyo leo watashinda bila wasiwasi wowote ni suala la muda tu.

"Tunaisheshimu Singida United, ila historia inatubeba, Namfua ni sehemu yetu ya kutangaziwa ubingwa na tuna bahati nao hata msimu uliopita wakati tuwanawafuata tulitangazwa kuwa mabingwa, hivyo leo historia itajirudia.

"Licha ya kutangazwa kuwa mabingwa bado tulishinda kwa bao 1-0 lililofungwa na Kapombe (Shomari) hivyo sioni tatizo katika hilo tunahitaji ushindi na kujikusanyia pointi tatu," amesema Manara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic